Kwanza nampongeza mmiliki kwa kukopa pesa na kujenga shule ni jambo jema sana, angeweza kujenga ''night club'' au ''casino'' na angepata pesa nyingi tu na kulipa mkopo, lakini watoto wetu wangapi wangeharibika kutokana na biashara hiyo ya casino? Hivyo basi hatuna budi kumsaidia mmiliki japo kimawazo.
Kwanza, ningeshauri serikali kupitia halmashauri kuiendesha hiyo shule kwa ubia kama sio kuinunua kabisa, ili kumpa muda huyu mama kujipanga upya katika wazo lake jema la kuelimisha watoto wetu.
Pili, wakae na bank waone ni namna gani watalimaliza tatizo hili, kama bank wanatoa mapesa kwa mpango wa huduma za jamii ''csr'' iweje wapige mnada shule bila huruma.
Tatu, mmiliki atafute wabia kama kanisa katoliki, bakwata, si vibaya hata akamtafuta mengi au yusuf manji.
Nne, apige magoti kwa lowasa amsaidie kuendesha harambee itakayosaidia kumaliza kama sio kupunguza deni hili na hatimae kuwaondolea msongo wa mawazo watoto wanaosoma pale.
Tano. Wamiliki watafute management consultant waweze kuibadili na kuwa kampuni hatimae wasajiri hisa zao katika soko la mitaji ''dse'' hii itawasaidia kupata wanahisa wenye weledi wa kuendesha mradi kwa ufanisi zaidi.
----------
Sent from my Nokia phone
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments