[wanabidii] MAANDAMANO YA WANACHAMA WA CHADEMA UBUNGO KUMPINGA JOHN MNYIKA

Thursday, July 17, 2014

Wanachama kadhaa wa Chadema jimbo la Ubungo wamepanga kuandamana kupinga kile wanachodai kua ni ubaguzi kwa kuwaondoa madarakani viongozi wa jimbo ambao wanamkosoa mbunge wao John Mnyika kutokana na mwenendo wake mbovu jimboni.

Viongozi hao ambao wameondolewa madarakani kwa shinikizo la mbunge John Mnyika ni pamoja na Eric Ongara "m/kiti" John Nkya "katibu" Suleiman Mfua" k/mwenezi" na Gerlad Kipanga "m/hazina"

chanzo cha kuondolewa kwenye uongozi viongozi hao ni misimamo yao kuhusu proglam ya Chadema msingi ambayo inaendeshwa kinyume na maelekezo ya Makao makuu ya chadema. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu wa karibu na viongozi hao ambao wanaheshima kubwa ndani ya chadema jimbo la ubungo kua baadhi ya viongozi wanatarajiwa kujiunga na vyama vingine vya siasa ambapo kwa upande wa ccm wanaotarajiwa kujiunga na chama hiko ni Eric Ongara pamoja na Gerlad Kipanga kwa upande wa A.C.T anaetajwa kujiunga na chama hicho kipya cha siasa ambacho kimetokea kua mwiba mkali kwa chadema ni Suleiman Mfua, kijana anaetajwa kua ni kipenzi cha wanachadema wengi wa jimbo la Ubungo kwa utendaji wake ndani ya Chadema.

Kufuatia hali hiyo makundi kadhaa ndani ya chadema Ubungo yameibuka yakipinga uonevu huo waliofanyiwa viongozi wao kwa shinikizo la Mbunge Mnyika.

HAYA SASA MAKAMANDA MWISHO WENU UNAKARIBIA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

Previous
Next Post »
0 Comments