[wanabidii] Askofu Valentino Mokiwa Ashitakiwa kwa Kumshika Makalio Mchungaji Mtikila

Wednesday, July 16, 2014

Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi kumshitaki Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Anglican.

Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.

Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo ufisadi wa au wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Iringa.

Mtikila alivyoitwa na Askofu kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nocholas, usiku wa saa 03:00.

Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti, kazi ambayo aliifanya yeye baada ya kufunga mlango.

Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.

"Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha.

Alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipepesa sehemu za siri za mlalamikaji".

Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha. Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo

Kesi inataarifiwa kuwa kwenye Mahakama ya Kisutu, chini ya Hakimu Mchome.

SOURCE: AMANI
DATE: TODAY
PAGE: 02,03

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments