[Mabadiliko] Je, ni halali 'mfumo kristo' kubugia futari ya waislamu?

Tuesday, July 08, 2014
Kuna hoteli moja karibu na hapa maskani kwangu inapika futari mujarabu sana. Mimi na rafiki zangu wakristo tumezoea kila siku kwenda kupata futari kwenye hoteli hiyo. Kwa kweli baada ya kugundua utamu wa futari hii nimeacha kabisa kula ugali/wali mpaka mfungo uishe. Ila kuna tatizo moja ambalo linanifanya nihisi kama tunawakosea adabu ndugu zangu waislamu. Mara nyingi wenzetu waislamu wakitoka kuswali swala ya magharibi wanakuta tumefukia futari lote limeisha.
 
Nimejaribu kufanya utafiti wa watu wanaoenda kufuturu pale nimegundua 60% ya wafutruruji ni wakristo. Na wakati ndugu zetu wameinama msikitini wakiswali muda huo ndio utakuta wakristo wamemiminika kwenye hoteli hiyo 'wakifuturu'. Pindi ndugu zetu wakitoka msikitini, hukuta 'mfumo kristo' tumemealiza 'futari yao'. Nimetafakari hili suala nikaona kwamba sio vema sisi wakristo kuvamia chakula kisichotuhusu na kuwakosesha wahusika.
 
Lakini kwa upande mwingine nafikiri kwamba hili linaweza lisiwe kosa kwa kuwa hiki ni chakula cha hotelini—kila mwenye fedha zake (bila kujali dini, kabila wala rangi) anayo haki ya kula msosi huu. Hata hivyo kabla sijafikia hitimisho la ama kuacha kumaliza chakula cha watu, imebidi nitumie fursa hii kuomba maoni/ushauri isije ikawa tunatenda kosa bila kujua. Je, ni halali sisi 'mfumo kristo' kuvamia chakula cha wenzetu na kukila chote huku wao wakikosa?
 

Share this :

Related Posts

0 Comments