Fw: [wanabidii] Zanzibar - Koloni la Tanganyika

Tuesday, July 08, 2014


On Tuesday, 8 July 2014, 9:13, 'Mike Zunzu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Sitofahamu kama jibu langu litakuwa jazi kwako!
Uliyoandika yawe na ukweli au laa, siwezi kuelewa, kama yana ukweli, na tatizo likaoneka ni katiba, nafasi ya kutunga katiba itakayoprekebisha palipo na hitilafu imepatikana, wawakilishi wa Zanzibar walio wa jumbe wa CCM wakaja kukaa kikao kimoja na wenzao wa bara wakaamua waende na msimamo ya kutokubali kubadirisha mambo yanavyokwenda, na wakakubaliana kwa kauli moja. Msimamo wa hao unaowaita wananyonywa wanatetea kwa hali na mali utaratibu huo uliopo uendelee. Unaposema Zanzibar inanyonyonywa,  je inanyonywa kweli au ni makelele tu wa watu walioshiba na kuanza kupayuka?
Kitu gani kimewazuia wabunge wa Zanzibar kuingia na kauli moja ya Kizanzibar, ili kimoja kieleweke, kama kunaunyonyaji wa aina yoyote basi ufanyiwe marekebisho, kama wamekaa kimya inamaana maneno yako hayana ukweli, maana wao, wengi wao wakiwa ni watumishi wa serikali wanafahamu mengi kuliko mtu baki.
Hadi sasa siamini kama kunaunyonywaji wa aina yoyote, na kama upo inamaana viongozi na wawakilishi wengine wanafaidika na unyonywaji huo, ukibadili mfumo inawakatia mrija. 
Kwa ujumla kosa haliwezi likwa la Serikali ya Muungano kana ulivyoiita, ili kuziba jina la Tanganyika.


On Monday, 7 July 2014, 19:49, 'Ngupula GW' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Kabla ya yote,jiulize kwa nini watz wanadai tanganyika...kabla hujajiuliza zanzibar inadhurumiwa nin na muungano jiulize zanzibar inachangia nin ktk gharama za muungano...forum hii tumechoka kujadili malalamishi ya zanzibar na isingekuwa masuala ya alshabab na boko haram tungewatimulia mbali...fed up in deed...ngupula

'ANDERSON ZAKARIA' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Mawazo yako mazuri lakini umesahau serikali ya muungano inavyonyonywa na Wazanzibar , kwa mfano gharama za umeme , ulinzi, na kadhalika, usikurupuke na hoja yako hii kwani haibebi maji.

Ole Zakaria


On Monday, July 7, 2014 8:18 PM, 'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Kwa mujibu wa utafiti yakinifu nilioufanya, nimegundua kwamba kuna mambo ya msingi ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ambayo Tanganyika imekuwa ikiinyonya Zanzibar na hatimaye kuigeuza kama koloni lake kwa muda wa zaidi ya miaka 50 ya Muungano! Nitafafanua baadhi ya mambo hayo katika uzi huu ili kuuweka ukweli huo bayana.
 
ANGALIZO
Naomba tujadiliane hoja hii kwa nidhamu na kwa ufasaha, bila ya jazba wala mihemuko yoyote ili hatimaye tufikie muafaka utakaokomesha unyonyaki huu ili wazanzibar wasiendelee kunyonywa na watanganyika tena.
…………………………………………………………………
Katika Muungano huu, Zanzibar ilikabidhi sehemu muhimu ya mamlaka yake (mahusiano ya nchi za nje, ulinzi na usalama, uraia, kodi na ushuru, sarafu, nguvu kuu za kuendeshea uchumi na mengineyo) kwa Tanganyika; na kisha Tanganyika ikajigeuza jina na kujiita Jamhuri ya Muungano.
 
 
Muungano huu ni kielelezo cha unyonyaji na ukandamizaji mkubwa ambao nchi ndogo ya Zanzibar imefanyiwa na nchi kubwa ya Tanganyika. Ni mfano wa jinsi ambavyo nchi moja kubwa ya Kiafrika inaweza kuigeuza nchi nyingine ndogo ya Kiafrika kuwa koloni lake.
 
Kwa miaka mingi Zanzibar imelalamika kwamba inapunjwa katika mgawanyo wa mapato yanayotokana na fedha zinazotolewa na nchi wafadhili na taasisi za kimataifa kwa Jamhuri ya Muungano. Sio tu kwamba Zanzibar haipati stahili yake ya mapato yanayopatikana kwa jina la Jamhuri ya Muungano kutoka vyanzo vya nje, bali pia fedha zinazopatikana kutokana na mambo ya Muungano zinatumika kwa mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika.
 
Jambo chengine ni kuhusu his --
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


Share this :

Related Posts

0 Comments