Hivi karibuni kuna tapeli la mtandaoni liloibuka ndani ya mitandao ya kijamii akitambulisha kama msichana ambaye akufata inbox na kukuomba uhusiano wa karibu na wewe hasa kwa wanaume kisha kuwarubuni kwa maneno ya kutunga hadi kupelekea kuwatapeli bila kujijua.
KISA CHANGU JUU YA TAPELI HILI.
Siku chache zilizopita kuna mtu alinijia inbox kwangu akiomba kuwa na urafiki wa karibu na mimi huku akitumia lugha ya kiingeleza na alikuja kwa page yenye jina la BLESSING KONEH. Cha ajabu baada ya mimi kumkaribisha hakutaka kuni-add na badala yake alikazana kuja inbox na akanyambia kuwa ana inshu ya siri anapenda kunishirikisha hivyo nimtumie email yangu kwani hapa Facebook alidai ni puplical hivyo inshu hiyo inafaa kuongelewa private sababu ni ya siri kuhusu maisha yake. Nilimkubalia nikamtumia email yangu na siku iliyofuata akaja kunitumia ujumbe kwenye mail akitumia email ya "blessingkoneh@ymail.com"
Katika ujumbe wake alinieleza kuwa yeye ni binti mwenye umri wa miaka 23 raia wa Ivory Coast. Akasema alikua na baba yake OLIVER KONEH ambaye alikua akifanya kazi kama mshauri wa kigogo wa serikali yao (kigogo huyo alimtaja akisema ni marehemu kwa sasa jina sikumbuki) ambaye aliuwawa na waasi mwaka 2009 asubuhi moja amabayo waliivamia nyumba yao na kumwu ua baba pamoja na mama yake, na yeye akaponea chupuchupu hivyo alikimbilia nchini senegel kwa hifadhi akiwa kama mkimbizi kwenye kambi ya Dakar kutokana na machafukao ya vita vya wenyewe kwa wenyewe (civil war) nchini mwao. Na ndugu zake walikimbilia katika mataifa ya kati ya Afrika, hivyo huko senegal hakuwa akimjua mtu zaidi ya mchungaji aliye mtaja kwa jina la Rev. ANDREW KUMA. Alinipa namba za huyo mchungaji na kunyambia kama ninge hitaji kuongea nae basi nimpigie alafu mchungaji atampelekea simu niongee nae.
Pia aliniomba msaada wangu, ambapao alinyambia kuwa alikua na vyeti vya kifo, taarifa za ki-benki na nyaraka za siri za baba yake ambaye alisema kuwa kabla ya kifo chake aliacha kitika cha pesa kipatacho $ 2.5 Mil. hivyo akaniomba nimtumie namba za account yangu ya bank ili aweze kuzisafirisha kutoka UK (uingeleza) ambapo pesa hizo zipo hadi kwenye account yangu akidai kwamba yeye kumiliki pesa akiwa kama mkimbizi ni kinyume na sheria za inchi hiyo.
Akanieleza kuwa katika pesa hizo nitamtumia kiasi kidogo ili aweze kusafiri kutoka huko aliko hadi kuja huku nilipo ili tuonane. Pia alinitumia na picha yake (Hiyo hapo pichani) huku akiomba kujua zaidi kuhusu mimi na shughuli nifanyazo. Akasisitiza kwamba hizo ni siri amenipa kutokana na kuniamini hivyo nisizivuje kwa watu kwani anahofia maisha yake. Alimaliza kwa kusema anapenda watu waaminifu na waelewa.
Siku ya jana ndiyo nilijibu email yake, nilikua na hofu sababu nilishasikia mambo ya ajabu ajabu yanoyotekea kwenye hizi social media. Basi sikutaka kukurupuka kwa mtu nisiye mfahamu nikamjibu kwa kumwomba ajieleze zaidi kuhusu amisha yake yalivyo kuwa na namna alivyozipata hizo documents za baba yake. Nikamwambia pia mimi ni mwanafunzi na bado niko chini ya malezi ya wazazi.
Sasa toka jana hadi leo nilipo mpandia inbox nikakuta jamaa kani-block nadhani sababu labda ya kumwambia kuwa mimi ni mwanafunzi na bado niko chini ya wazazi.
Leo katika feeding zangu humu Facebook ndo nimekutana na habari zake kwenye page ya BONGO SWAGG nkashtuka kukuta kisa ni kile kile kama changu.
Kumbe tapeli hili licha ya kutumia majina ya kike lakini jina lake halisi ni SIMON ABUSH na anatafutwa kote duniani kwa kuishafulia jina benki ya HALIFAX FINANCE MANAGEMENT BANK OF LANDON ambako anadai pesa hizo zipo.
[[kotasini]] Chukua tahadhari usije ukajiingiza matatizoni pia kujipa hasara kwa kumwamini mtu usiyemjua. Pia uweza pia ku-share post hii ili kuwafikishia taarifa rafiki zako ambao wako hatarini kwa watu wa aina hiyo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments