[wanabidii] Tabia ya Waandishi wa habari kuwa-blackmail watu mitaani

Tuesday, June 03, 2014
Imezuka tabia chafu miongoni mwa waandishi wa habari ya kuwa-blackmail watu mitaani. Juzijuzi mwandishi mmoja (jina nalihifadhi kwa sasa) alitaka apewe Shilingi milioni 2 na ndugu yangu ili asiandike habari zake alizodai ni 'mbaya'. Mwandishi huyu mshenzi alijitambulisha kuwa anatoka kwenye gazeti ambalo mhariri wake ni rafiki yangu. Nilipompigia simu mhariri na kumuuliza iwapo ana mwandishi anayeenda kwa jina hilo alisema huyo huwa anachangia tu makala kwenye gazeti lake na sio mwajiriwa. Alishangaa sana nilipomueleza kisa kizima, na alishauri tumuwekee mtego. Ana bahati sana mshenzi huyu! Nimeambiwa wapo waandishi wa habari wengi 'feki' wanaojihusha na mchezo huu mchafu. Nasema ole wao! Nafanya mawasiliano na Jukwaa la Wahariri na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ili, pamoja na mambo mengine ya kusimamiaa taaluma, waweze pia ku-deal na washenzi wa aina hii wanaochafua sifa nzuri ya wanahabari.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments