Ni muda sasa tangia nione tukio la kuhama kwa ofisi ya serikali ya mtaa toka eneo lake na kwenda katika nyumba binafsi kwa bwana Mbise..Nilidhani labda kuna matengenezo yanataka kufanyika katika jingo lile au eneo zima kwa ujumla wake.Kilichonifanya nije hapa ni taarifa ambazo nimezisikia jana toka kwa baadhi ya wenyeji wa pale nilipopita eneo lile,ambazo zimenishtua kuwa eneo hilo inaonekana linauzwa kijanja na wajanja tuliowapa nafasi ya kutuongoza na ikibadilishwa toka serikali ya mtaa na kuonekana mwenye umiliki ni Ndugu Kibati.
Nikaona si vyema kuiacha mali ya umma inatafunwa na wajanja kama ni kweli taarifa hii,hivyo wananzengo natarajia kupata watu hapa ambao labda wana ufahamu mpaka kuhusiana na eneo lile kwa sababu nilipojaribu kuwahoji wenyeji waliokuwa wakijadili suala hili ili nipate ukweli wa kutosha na historia ya eneo husika walionekana kuwa waoga na kukataa katakata kusema chochote kwa madai ya kuogopa kutolewa uhai na hao wanaojimilikisha,wakashauri nifuatilie kwingine taarifa hizo.
Kwa heshima na taadhima niwaombe wale wanaUkonga ambao ni wadau wa ofisi ile na wanajua kwa undani sakata la ofisi ile na hata wengine walishiriki kujenga kwa kuchangia na hata nguvu zao waje hapa kutujuza ukeweli na hata waandishi wa habari ningeomba waende pale kujua nini kinaendelea katika ofisi ile.Pamoja na hilo ningemuomba diwani wa eneo Mtahiki Mayor wa Ilala Jerry Slaa pamoja na Mbunge wa pale japo si muwajibikaji kwa asili yake huyu ni Mh. Eugen Mwaiposa waje hapa kutujuza kama wanafahamu kinachoendelea pale.
Bila kuwakatalia watawala wanaweza wanaweza kuuza chochote na kwa sababu yoyote.Endapo watanzania tutaamua kukaa kimya huku tukiwapigia makofi bila kuhoji basi siku moja tutaja kustuka kama watokao usingizini na kuulizana hivi kile ama hiki na hata kile kiliuzwa lini?Isije kuwa kama UDA maana mgogoro wa kimaslahi kama usingetokea miongoni mwa watawala wetu basi tusingejua leo na kelele hizi usingezisikia.Kama si mfuatiliaji ili ujue Fulani na Fulani waliiba kwa Fulani ni mpaka wakidhurumiana walichoiba la kama wamegawana kwa kuridhika hutajua na hukaa pamoja kuandaa wizi mwingine zaidi,hivi ndivyo hata baadhi ya watawala wetu wasio waaminifu walivyo ndani ya serikali yetu.
Nawakaribisha tufuatilie hili na kuujua ukweli……..
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments