[wanabidii] Majibu ya Dr. Slaa kwa mwanachama kuhusu kukwepa mazishi ya Mama Zitto

Wednesday, June 04, 2014
Majibu ya Dr. Slaa kwa mwanachama kuhusu kukwepa mazishi ya Mama Zitto

Wadau,

Katika ufuatiliaji zaidi nimegundua kwambakuna mwanachama wa CHADEMA ambaye aliguswa na kisa cha viongozi wakuu wa chamakususia mazishi ya Shida Salum aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Mwanachamahuyo baada ya kuumizwa na kitendo hicho cha viongozi wake, alimwandikia smsifuatayo Dr. Slaa.

Nimeihariri ili kuondoa vifupisho vya maneno alivyovitumia ili kila mmoja aelewe:
"Kweli baba wewe na Mbowe mmeshindwa kabisa kushiriki mazishi ya mjumbe wa kamati kuu!! Ninyi hamna kabisa utu hata chembe? Sababu za kisiasa zimewafanya muwe na mioyo migumu kiasi hicho? Utadhani nyinyi hamtakaa mfe milele?

Mmeshangaza ulimwengu, ubinadamu kwenu siyo kitu kwa ajili yasiasa? Hivi wewe utakuwa mwanasiasa milele? Kweli hamna hata hata hofu ya Munguhata kidogo, hata wewe ambaye ulikuwa mtumishi wa Mungu kweli baba? Hata kamani ubabe, wa kwenu haujawahi kutokea.

Hata kama Zitto hayuko CDM mchango wakekatika kujenga chama mmeusahau kabisa? Mmelipa kisasi kwa kususa hata maiti! Kwa ajili ya siasa tu! Duh! Hongereni, fanyeni siasa milele. Watu wenye hekimawamepata somo toka kwenu. Mungu awabariki sana".

Mwisho wa kunukuu.

Sasa soma majibu ya mtu anayeitwa Dr.Willibrod Slaa ambaye kama kura zingetosha mwaka 2010, eti leo angekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sms yake imetoka kwenye namba yake ya 0783967519 na ili-deliver kwenye simu ya huyo kijana saa 18:40:27 jana Jumanne tar 2/6/2014. Nainukuu sms hiyo bila kuhariri chochote:

"Acha ushabiki usiokuhusu. Makamu Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA, mhe. Issa Mohamed alifiwa na mama yake mzazi siku 7 zilizopita. Nani alihudhuria, mbona hata wewe hukuhudhuria! Wala hukuandika sms kama hii, kumbe Utu wako unapimwa kwa fulani tu! Upuuzi. Chadema haifanyi siasa ya misiba. Utu unapimwa uliyomfanyia mgonjwa siyo kwenye mitandao na magazeti. Fanya utafiti kabla ya kujifanya mjuaji. Dr Slaa"

Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye rais wa UKAWA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments