[wanabidii] Madudu ya Uchaguzi Mkuu wa CUF haya hapa

Thursday, June 19, 2014

Wadau, amani iwe kwenu.

Kama ilivyoamuliwa na baraza Kuu la chama, uchaguzi wa viongozi wa juu wa Chama cha Wananchi ( CUF ), ulitarajiwa kufanyika tarehe 22 Juni 2014. Katika uchaguzi huo, Katibu Mkuu Seif Sharif Hamad alihakikisha kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti ni Prof Ibrahim Haruna Lipumba na mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Mkuu ni mwenyewe Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika hali nyingine isiyokuwa imetarajiwa na inayoleta utata ni kwamba, Maalim Seif Sharif Hamad alipendekeza kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti igombewe na Juma Duni Haji badala ya Makamu Mwenyekiti wa sasa Machano Othman ambaye kwa upande mwingine ndiye anayeungwa mkono na Ibrahim Lipumba. Maalim anafanya hivyo akiamini kwamba yeye akishirikiana na Duni wataongeza nguvu ya kumdhibiti Lipumba. Wawili hao Maalim Seif na Duni Haji hawataki Lipumba agombee tena Urais na wameshamshauri agombee Ubunge Jimbo la Temeke kwenye uchaguzi Mkuu wa 2015. Juma Duni Haji ndiye aliyepangwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi wa 2015.

Halikadhalika, Maalim Seif Sharif Hamad anataka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu igombewe na Joram Bashange, Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Bukoba badala ya Julius Mtatiro ambaye hamtaki kwa sababu anambana Maalim Seif Sharif Hamad katika masuala kadhaa ya kiutendaji ya chama hicho. Sababu ngingine ya Maalim kumuogopa Mtatiro ni hisia kwamba yeye ni pandikizi la CHADEMA.

Aidha, katika kupingana na maamuzi ya Baraza Kuu, Maalim Seif Sharif Hamad ameagiza uchaguzi huo ufanyike tarehe 27 Juni 2014. Sababu ya kusogeza mbele ni jitihada za maalim Seif kupanga safu yake ya uongozi na kuwaweka wagombea dhaifu ambao watakaopambana nao. Katika kufanikisha hilo, nafasi ya Mwenyekiti itagombewa na Prof Lipumba ambaye atapambana na Chifu Rutanyosha ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Shinyanga. Kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu, Maalif Seif amejipangia kupambana na mwanachama wa kawaida Adam Bakari kutoka Temeke. Kiini macho hiki kimeandaliwa ili kuwahadaa Wanachama na Watanzania kwa ujumla kwamba uchaguzi wa ndani ya chama hicho umefanyika kidemokrasia.

Makamu Mwenyekiti wa sasa Machano Othman ameshinikizwa ajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho na nafasi yake itachukuliwa na Said Abdallah kutoka Micheweni. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu itachukuliwa na Joram Bashange kama nilivyoeleza hapo juu. Hii maana yake ni kuwa Julius Mtatiro amekalia kuti kavu ndani ya CUF na soon atatangaza maamuzi magumu ya kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

Wadau, mnajionea wenyewe jinsi vyama hivi vinavyojiita vya upinzani ambavyo vina ndoto ya kuing'oa CCM vilivyo na siasa za kinafiki na kilaghai. Yaani mtu mmoja tu ndiye huamua nani agombee na nani asigombee. CUF mungu mtu wao ni Maalim Seif, CHADEMA yupo mzee Edwin Mtei na NCCR yupo James Mbatia. Hakika kwa mwendo huu kuitoa CCM madarakani ni ndoto za mchana.

Nawasilisha

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments