Na Happiness Katabazi
WAKAZI wawili wa Tabata Jana wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Dar es Salaam KWA makosa ya kukutwa na meno ya tembo ya sh.milioni 275.5 bila kibali.
Mbele ya Hakimu Mkaz Waliarwande Lema Wakili wa serikali Ofmedy Mtenga aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni Dominick Kombe (36) mfanyabiashara na Herbert Machaka (30) mkulima.
Wakili Mtenga Alida kuwa washtakiwa wanakabiliwa na shtaka mmoja na uhujumu uchumi na kuwa Juni 5 mwaka huu, washtakiwa wakiwa eneo la Tabata Kisukuru walikutwa na meno ya tembo vipande 28 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba vipande hivyo vina thamani ya dola za kimarekani 165,000 sawa na sh. milioni 275.5 za kitanzania bila kibali.
Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa apate dhamana nilazima kila mshitakiwa awe na mdhamini mmoja atakaye saini sh. milioni 10 au mali isiyohamishika yenye zaidi ya sh. milioni 10.
Hakimu Lema alitoa masharti ya dhamana, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati ya kuruhusu mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo.
Ki utaratibu kesi za uhujumu uchumu zinasikilizwa Mahakama Kuu,lakini kama DPP akiwasilisha hati kuruhusu mahakama hiyo kusikiliza basi Mahakama itasikiliza. Wakili huyo alidai upelelezi haujakamilika. Kesi hiyo itatajwa Julai 9 mwaka huu.
Wakati huu huo Raia wa wa Burundi Vanessa Shuwejimana (19), ambaye alikutwa akijiuza eneo la hoteli ya Clinton,Dar es Salaam amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya sh. 100,000 kwa kuishi nchini bila kibali.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Juni 25 Mwaka 2014.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments