[wanabidii] CHADEMA wanaua vipaji vya siasa kwa Vijana, Yu-wapi James Ole Milya na Bananga

Tuesday, June 17, 2014

Miongoni mwa sifa mbaya ambayo chama cha demokrasia na maendeleo imejiwekea ni pamoja na kuua uwezo na umakini wa vijana wake ili viongozi wa juu wa chamq hicho waendelee kuenjoy kushikilia nafasi zao bila kuwa challenged, kwanu kama ilivyo kawaida ya kimaumbile kijana ni mtu mwenye kupenda critics hasa kijana huyo akiwa msomi anayejitambua anakuwa tishio zaidi kwa viongozi ambao hawana elimu na wasiojielewa.

Kwa kutambua ukweli huo Viongozi wa Chadema wamekuwa na historia ya kuwatumia vibaya vijana kwakuwafanya wasifikiri na kuwaburuza na kisha kuwapoteza njian vijana hao.

Historia inatuonyesha kuwa kila kijana makini aliyejitambua ambae alionyesha kipaji na kipawa ndani ya CHADEMA hakuwahi kudumu sana. Miaka ya nyuma kidogo tuliona vijana makini makini kama Kafulila wakitimuliwa kwa aibu ili iwe fundisho kwa wengine wanaotaka kuhoji.

Lakini mbaya zaidi hata wale vijana active na wanaoonesha vipawa kwenye uongozi hawana safari ndefu kwenye siasa za Chadema wanazimika ghafla.

Kila kijana utakayemtaja wa CHADEMA ya leo ni mzigo unaoburuzwa na kuambiwa nini cha kusema na kufanya. Mnyika wa leo sio yule wa zamani, hivyo hivyo kwa mdee na vijana wengine walioonesha vipawa katika siasa ndani ya chama hicho wamekuwa wakinyamazishwa kimya kimya. Bavicha ndo kama vile haipo kabisa, hakuna kinachoendelea wala kijana anayesikika.

Katika kipindi cha miaka ya karibuni kulikuwa na nderemo nyingi katika chama hicho kwa ujio wa vijana kutoka CCM, James Ole Milya na Ally Bananga ambao walikuwa viongozi wa UVCCM ngazi ya mkoa. Lakini kama ilivyo kwa vijana wengine waliowahi kujiunga na chama hiko kwa mategemeo makubwa namatumaini hawajulikani walipo. Chama hicho kimewa-dump vijana hao ambao walionyesha ukinara katika siasa hapa nchini.

Kimsingi hakuna kijana YEYOTE aliyefanikiwa kisiasa ndani ya CHADEMA isipokuwa wale wabeba viatu wa viongozi wakubwa wa chama, wale wote ambao wameonyesha uwezo binafsi wamepotezwa.

HAKIKA CHADEMA inaua vipaji vya siasa kwa Vijana wake. Ni chama cha ajabu sana kuwahi kutokea duniani, wakati vyama vingine vinaimarisha taasisi zake za Vijana na Jumuiya ili kuwa na better succession plan Chadema wanaua vipaji vya vijana ila viongozi wa juu waendelee kubaki wenyewe...hivi kwa mfano nikiuliza swali la kichokozi ni nani mbadala wa Mbowe na Slaa chadema..? Nani anaweza kunipa jibu lenye uzito hata kidogo..? Naijua chadema hakuna huyo mtu, hakuandaliwa na hatoandaliwa. Wamebaki vijana wachumia tumbo, wa ndio mzee mazuzu yasiyojielewa.

Chadema endelezeni Vijana wenu, capacity building ni muhimu kwa uhai wa taasisi yeyote hata ikiwa ni SACCOS ama VICOBA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments