[Mabadiliko] Tahadhari kwa Waegeshao Magari Jijini Dar

Friday, June 27, 2014
Kutoka kwa Taji Liundi

TAHADHARI: Inanisikitisha sana kuandika tahadhari hii kwenu rafiki zangu. Haistahili kuwa tahadhari. Lakini SASA HIVI katika mitaa mbalimbali jamaa zetu wa TANROADS wanapita kukamata na kupiga FINE magari yaliyoegeshwa "vibaya".
Fine ni Tsh 220.000.
Hili ni tatizo kubwa sana na RUSHWA inafukuta kwenye zoezi hili. Mtanzania wa kawaida HAWEZI kulipa kiasi hicho kama ameegesha KANDO YA BARABARA zetu za kawaida, mfano pale Sinza Palestina.
Hao jamaa wanadai inabidi uwe umewasha TAA ZA TAHADHARI NA UWEKE TRIANGLE.
Sawa. Lakini si kawaida kabisa na zoazoa yao leo ni hatari. Wanatembea na Noah kubeba madereva/abiria waliokamatwa.
MAONI YANGU: Tusinyanyasane! Sio uungwana. Wananchi tunasota ile mbaya. Huko mitaani tunahangaika kujikwamua kiuchumi.
TANROADS kama Wakala wa Serikali inatakiwa ITOE MATANGAZO YA ELIMU KWA UMMA KABLA YA KUCHUKUA HATUA ZA KISUMBUFU NA KIHALIFU KWA KUCHOCHEA RUSHWA(wanakubali hadi Tsh 60/70elfu ukiongea nao).
Kwa kawaida, wangetakiwa wapite hata na PA watangaze: "Ndg wananchi katika eneo hili, mnaombwa kuegesha magari yenu kwa utaratibu huu kandokando ya barabara kuu. Hakikisha umewasha taa za dharura na weka Triangle mita...nyuma ya gari".
Hii ingeondoa usumbufu wa KUMWELEKEZA kila mkosaji.
Tumieni TBC!! RADIO Uhuru nk. Ombeni Matangazo ya kijamii kwenye Radio binafsi.
Kinachotokea ni shambulio la kihalifu kwa WaTanzania wasio na hatia. Kwa mara nyingine tena naandika kuhusu uendeshaji mambo KIHOLELA. Uholela huu unanyanyasa waTanzania.
Marafiki zangu humu mlio na wadhifa na uwezo wa kufwatilia hili..fanyeni hivyo. Mtagundua nazungumza UKWELI!!
Sijapendezwa!
Eneza TAHADHARI hii.

--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAC1jnjdS-ncdWJSMLN12fP-U%3DPzCZwdBprxxqN1g7apJxa8Gew%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments