WANAOTISHA WENZAO KUHUSU PANYA ROAD/MBWA MWITU
Ndugu zangu ,
Kuna rafiki yangu wa Kike amenipigia simu muda mchache uliopita kuniuliza kuhusu hawa PANYA ROAD na MBWA MWITU .
Kwamba eti ni tishio kubwa kiasi kwamba hata nae anaogopa kurudi nyumbani muda huu mpaka atakapohakikishiwa usalama wake .
Nilipojaribu kumhoji Zaidi akaniambia anaishi maeneo ya kinyerezi , Huko kinyerezi kulivamiwa na vijana hawa wa Panya Road leo hii , na kufanya madhara kadhaa .
Mie nilimwambia asiwe na wasi wasi na nikampa namba za dharura kupiga endapo chochote kitatokea eneo alipo na ataweza kushugulikiwa .
Wakati najadiliana na huyu mwingine aliniambia ndugu zake wanaogopa kurudi kwao maeneo ya segerea kwa sababu ya hawa vijana wa Mbwa Mwitu na Panya Road .
Muda wote nimewapa namba za mawasiliano za polisi makao makuu , kuripoti chochote katika maeneo yao na askari watafika eneo hilo mara moja ila wasijichukilie sheria mkononi .
Wahalifu wanatakiwa kwa ajili ya mahojiano na kazi nyingine za kiusalama ili kuweza kuthibiti uhalifu wenyewe ila ukiuwa tu ujue kuna chembe Fulani za ushahidi umepoteza na saa nyingine unatengeneza uadui na watu wengine Zaidi haswa jamii za jirani kama mtu huyo ni wa maeneo hayo .
Pia tupende kutoa taarifa sahihi kuhusu matukio yanayotokea katika maeneo yetu na ikiwezekana kwenda kutoa ushahidi mahakamani bila kulazimishwa au kushawishiwa kwa rushwa .
Hili la Mbwa Mwitu na Panya Road linafanyiwa kazi , hata jeshi la polisi limetoa taarifa mara kadhaa kuhusu suala hili , ila wananchi nao wanasehemu yao katika kuhakikisha msako wa wahalifu hawa unafanikiwa kwa kutoa taarifa za ukweli na wazi bila kuogopa wala kushawishiwa na mtu .
Wanaowatisha wenzao kuhusu mbwa mwitu na panya road eti wasitembelee maeneo Fulani au wasirudi majumbani kwao kwa sababu ya makundi haya inaonyesha wana taarifa sahihi kuhusu hawa vijana , ni vizuri nao wakamatwe na kuhojiwe vizuri kuhusu vyanzo vya taarifa zao .
Huwezi kumtisha mtu asirudi kwake au kwao au asiende sehemu Fulani wakati serikali ipo , itaendelea kuwepo na haijatangaza hali yoyote ya Amani .
Institut d'études de sécurité - SA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments