BREAKING NEWS: WAKILI RUTAGATINA AREJESHEWA UWAKILI NA MAHAKAMA
Na HAPPINESS KATABAZI
WAKILI CHRISTIAN RUTAGATINA AMESHINDA RUFAA YAKE ALIYOKUWA AMEIKATA KATIKA MAHAKAMA YA RUFAA DAR ES SALAAM 2012. MAHAKAMA YA RUFAA IMETENGUA HUKUMU YA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YA SEPTEMBA 6 MWAKA 2006 NA HUKUMU YA KAMATI YA MAADILI YA UWAKILI YA MWAKA 2005 AMBAZO HUKUMU HIZO MBILI ZILIMTIA HATIANI RUTAGATINA KWA KOSA LA UTOVU WA MAADILI YA UWAKILI KWA KUMUOMTAKA MTEJA WAKE CLAVERY NGALAPA AMPATIE FEDHA ILI AKAWAPATIE FEDHA MAOFISA WA MAHAKAMA ILI WAWEZE KUMSAIDIA ASHINDE KESI.
MAHAKAMA YA RUFAA IMESEMA HUKUMU ZOTE HIZO MBILI NI BATILI KWANI ZIMESABABISHA RUTAGATINA AONDOLEWE KWENYE ORODHA YA MAWAKILI NA ASIFANYE KAXI YA UWAKILI KWA MIAKA TISA, NA KWAMBA TARARTIBU ZA KISHERIA ZIKIUKWA NA KWAMBA HUKUMU HIZO ZILIVUNJA HAKI YA KUMUHUKUMU BILA YA KUACHAKAZI MASHAKA.
HUKUMU ZILE MBILI ZILIACHA MASHAKA MENGI KWANI NGALAPA ALISHINDWA KULETA USHAHIDI WA MAJINA YA MAOFISA WA MAHAKAMA WALIOKUWA WANATAKA WAPEKEKEWE RUSHWA NA RUTAGATINA.
0 Comments