TAARIFA YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU NA BARAZA KUU LA CHADEMA NA VIONGOZI WA BARAZA LA VIJANA MIKOA YA GEITA, MWANZA, SIMIYU NA KAGERA .
UTANGULIZI:
Ndg.waaandishi awali ya yote nichukue nafasi hii kuwashukuru wote kwa mwitikio wenu katika kikao hiki muhimu kwa mstakabali wa Taifa letu kama nilivyo jitambulisha hapo huu mimi ni Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Geita pia kamanda wa Redbragete kanda ya ziwa na Mwenyekiti wa Makatibu wa Mabaraza kanda ya ziwa Magharibi. Nipo hapa kusoma maazimio ya wajumbe wa Baraza kuu, mkutano mkuu na viongozi wa Baraza la vijana la Chadema mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu na Kagera kupinga na kulaani kile kilichoitwa UKAWA.
UDHAIFU WA UONGOZI WA CHADEMA
Tunaungana na kuwapongeza wajumbe wenzetu wa mikoa ya PWANI, DSM na TANGA waliokemea upuuzi huu mapema wiki hii.
Kwa kweli suala hili halivumiliki na si la kulichekea hata kidogo.
Ndg.Wanahabari itakubukwa kuwa chama chetu ni chama makini kinachoamini katika nguvu ya umma na siyo nguvu ya viongozi sasa cha kushangaza hapa viongozi wetu wameendelea kutuburuza sisi wanachama na viongozi wa ngazi za chini bila kushirikishwa katika maamuzi ya chama.Kwa mfano kitendo cha ubabe wa M/Kiti wetu kuendelea kufikiri kwa niaba yetu na kufanya maamuzi peke yake ni kutudhalilisha sisi kama viongozi na watanzania kwa ujumla.
Tunalaani kwa nguvu zote kitendo cha viongozi wetu wa juu kufanya maamuzi ya kihuni na ya kifedhuri cha kususia bunge la KATIBA na sasa hivi kuanza kutoa masharti ya kitoto kwamba ili warudi Bungeni ni lazima yatekelezwe masharti hayo.
Tunasikitishwa na unafiki huu uliiopitiliza, viongozi wetu wamekubali kuwa sehemu ya matapeli wa kisiasa, wamekwenda kwenye BUNGE LA KATIBA wamekula posho zinazotokana na kodi zetu walala hoi, halafu wameacha kufanya walichotumwa.
Kuanzisha UKAWA na kususia BUNGE LA KATIBA ni muendelezo wa siasa za kinafiki, huu ni muendelezo wa mipango ile ile ya kuwahadaa Watanzania kupitia misimamo yetu isiyosadikika.
Njia bora na nzuri kwetu ni kupambana kupitia Hoja, na wabunge wetu wa katiba walipaswa pia kupambana kupitia Hoja na sio kukimbia Bungeni,
Kuungana na washirika wa CCM, ambao ni CUF na NCCR-MAGEUZI kwenye kufanya harakati hizi kunatupa wakati mgumu sisi wananchi na viongozi wa huku chini na Tunaamini kwamba kama imewezekana kwa viongozi wetu KUUNGANA NA CCM-B, kamwe haitashindikana siku moja MBOWE akituambia TUUNGANE NA CCM, na kwamba kwenye SIASA HAKUNA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU. Huu ni upuuzi na uzembe mkubwa wa kisiasa unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa.
Kususia vikao vya bunge la katiba kwa sababu tu SERIKALI TATU zinakataliwa na CCM, ni kudhihirisha kiasi gani kwamba viongozi wetu hawa ni WAROHO WA MADARAKA na kwamba wanataka kuutumia mchakato huu wa KATIBA MPYA kama ngazi yao ya kupata madaraka kiurahisi.
Kwanini CCM wao hawakususa na kutoka nje ya bunge baada ya kuona CHADEMA na CUF na wengineo wanapinga uwepo wa SERIKALI MBILI?. Kwanini tumewaruhusu wenzetu waendelee kupata platform ya bure kiasi hiki?. Viongozi wetu kwenye hili wameboronga na wanapaswa sio tu kujiudhuru lakini pia wanachapwe viboko hadharani kwa kutusaliti na kuzisaliti nafsi zao.
Tunapenda kuwakumbusha WALAFI HAWA WA MADARAKA, kwamba huku mikoani IDADI YA NAMBA ZA SERIKALI SIO AGENDA, huku kwetu tuna shida ya Mbolea, shida za ajira kwa vijana na jamii kwa ujumla, migogoro ya mipaka, mkiundo mbinu, Afya na nyinginezo, mmesusa kushiriki vikao vya kuandaa katiba nani atatusemea haya maswala kama kweli mnajiita UKAWA ni umoja wa katiba ya wananchi?. ACHENI UNAFIKI
kwa kuwashirikisha CUF na NCCR Kwenye kambi rasmi bungeni kwani sisi kuna viongozi wa chama ngazi mikoa na wilaya tuliwahi kuhoji pale vionozi wetu waliposema hatuwezi kuwashirikisha CUF na NCCR kwani wao ni CCM .B na sisi tuliamini hivyo na kuona CUF na NCCR ni kikwazo kwetu sasa tunashangaa leo bila hata kuja kwetu sisi kama viongozi na wanachama kuelezwa kilichoibadilisha CUF na NCCR ghafla kutoka kwa CCM B.na kuwa wapinzani lmala? Sisi wanachama na viongozi bado tunaamini CUF na NCCR bado ni CCM B. tena iliyo kubuhu.Hatukubali hatukubali kuungana na vyama vinavyotumiwa na CCM.
Tunalaani kwa nguvu kubwa ujanja ujanja huu wa kisiasa, hatuwezi kukubali kutumiwa kila siku na mabwana wakubwa hawa na sisi tuendelee kuwavumilia na kuwakalia kimya kila uchao, tunataka waache kuendelea kutufanya sisi viongozi wa chini kama mandondocha wa kisiasa kama walivyo wao.
HITIMISHO.
Sisi kama viongozi wenye machungu na chama chetu tunaonya na kulaani kitendo cha chama chetu kuungana na CUF na NCCR kwa sababu vyama hivyo vinatumwa na CCM. Hatuko tayari kuendelea kubaliki upuuzi kama huu wa viongozi wetu kutumwa na kujinufaisha na familia zao huku sisi tukiishia maisha ya kuhangaika iko taarifa ya viongozi wetu kuhongwa na CUF ili kudhoofisha upinzani Tanzania kwa mwendelezo uleule wa upinzani maslahi.
Tunawataka viongozi wetu hawa waitishe mkutano wa BARAZA KUU haraka iwezekanavyo ili tulijadili swala hili na ikiwezekana tuwawajibishe kwa kujitwisha madaraka yasiyo yao.
Mkutano huo wa Baraza kuu uitishwe haraka iwezekanavyo na usisimamiwe na Mbowe wala Dkt.Slaa na badala yake usimamiwe na BARAZA LA WAZEE LA CHAMA kwa kuwa Mbowe, Dkt. Slaa na waganga njaa wenzake kwenye hili wao ni watuhumiwa.
Vile vile Tunatoa siku kumi na nne viongozi wetu kujitoa mala moja ndani ya genge hilo la UKAWA ili kunusuru upinzani nchini.
na wanandeni warejeshe kwani kwa chama chetu maana imani tayari imeshaanza kupotea baada ya siku hizo 14 kupita bila utekelezaji wa matakwa ya wanachama tuliowengi basi tutashawishi na kanda zingine nazo ziungane nasi kususia kushiriki shughuli za chama ikiwemo migomo na maandamano.
Nawashukuruni sana kwa kunisikiliza
TAARIFA HII IMEANDALIWA NA;- wajumbe wa Baraza kuu na mkutano mkuu wa CHADEMA na wajumbe wa BARAZA LA VIJANA BAVICHA wa mikoa ya Geita, Simiyu, Kagera Na Mwanza.
Na limesomwa leo tqrehe 21.05.2014 hapa mkoani Geita nami
FIKIRI MIGIYO
………………………………
KATIBU WA BAVICHA MKOA GEITA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI TENDAJI BAVICHA TAIFA.
MWENYEKITI WA MAKATIBU WA MABARAZA YA KANDA YA ZIWA MAGHARIBI
MKUU WA REDBRIGADE KANDA YA ZIWA.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments