UTANGULIZI:
Jibu Maswali yafuatayo uzawadiwe kitabu kipya cha Richard S. Mabala kiitwacho 'Run Free'. Mshindi atakabidhiwa pia Cheti cha ushindi na mtunzi mwenyewe na kupata fursa ya kutoa mada kuhusu kitabu kwenye 'Mjadala wa Uzinduzi wa Kitabu' hicho unaoandaliwa na Taasisi za 'Kitabu Nilichosoma na Soma: Leisure Culture and Learning ambao unatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 17/05/2014.
Katika Kitabu cha 'Run Free' mwandishi amejikita katika kueleza umuhimu wa kuthamini vipaji vya watoto na kuviendeleza, kisa cha Wasichana marafiki Rehema na Clara kikisimama katika muktadha huo na kikishajiisha wajibu wa jamii katika kutoa fursa ya kujiendeleza katika michezo kwa watoto wa kike.
MASWALI:
Nchini wamekuwepo wanariadha kadhaa mashuhuri wanawake, Pichani ni Wanariadha wawili Wanawake mashuhuri mno katika historia ya Tanzania.
1. Taja Majina yao Kamili.
2. Taja 'baadhi' ya mashindano ya Olimpiki waliyoshiriki, maeneo yalipofanyika na miaka ambayo yalifanyika.
3. Taja Mwanariadha mwengine mwanamke wa Tanzania tofauti na wawili hawa.
MASHARTI NA MAELEKEZO MUHIMU YA SHINDANO:
Ili kushiriki shindano hili zingatia yafuatayo:
1. Zawadi itatolewa kwa mtu mmoja atakayetuma 'Comment' yenye 'majibu sahihi' MAPEMA KULIKO WATU WOTE.
2. Kabla ya kuandika jibu lako 'like' ukurasa wa 'Kitabu Nilichosoma' ili kukuza wigo wa ukurasa na kuchochea harakati za kuhamasisha usomaji wa vitabu.
3. Andika jibu lako kwenye 'comment moja tu'.
4. Ili kutofautisha'comments' za majibu na comments nyinginezo, anza jibu lako na kaulimbiu 'KITABU NI SILAHA'
5. Unaweza ku-edit jibu lako mara zozote upendazo lakini kumbuka muda utaorekodiwa ni wa marekebisho yako ya mwisho na si muda wa 'ku-post' (ku-comment) kwa mara ya kwanza.
6. Majibu yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili ama Kiingereza
7. Zawadi itakabidhiwa kwa mkono kwa mshindi wa kwanza siku ya Mjadala wa kitabu cha 'RUN FREE' unaotarajiwa kufanyika katika Mgahawa wa 'Soma Book Shop' jijini Dar es salaam. Kwa walio nje ya Dar es salaam watatumiwa huko waliko. Walio nje ya nchi watapendekeza wawakilishi walio nchini wa kupokea zawadi kwa niaba yao.
8. Mwisho wa kuandika majibu ni 'Saa Tano Kamili Usiku' siku ya Ijumaa tarehe 09/05/2014.
9. Mshindi atatangazwa kwenye ukurasa huu wa 'Kitabu Nilichosoma' saa nne kamili usiku siku ya Jumamosi (10/5/2014) baada ya majibu kupitiwa na jopo la majaji.
10. Ukurasa unaweza kuzawadia zaidi ya Mshindi mmoja kutegemeana na namna shindano lilivyokuwa.
KUMBUKA: ILI KUJIHAKIKISHIA USHINDI, UNAPASWA KUANDIKA MAJIBU YAKO MAPEMA!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments