TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka jana jioni tarehe 6 Mei, 2014 kuelekea Abuja, Nigeria kuhudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum).
Mkutano huo unaoanza leo tarehe 7 – 9 Mei, 14, utahudhuriwa na viongozi kutoka Afrika na duniani kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine mkutano utajadili njia mbalimbali zitakazolifanya Bara la Afrika kuumudu ukuaji wa kiuchumi kwa pamoja na fursa za ajira zinajitokeza.
Katika Mkutano huo, viongozi pia watajadiliana jinsi ya kugharamia
miundo mbinu Barani Afrika, njia za kukuza biashara baina ya nchi zao na uwekezaji katika sekta ya kilimo barani.
miundo mbinu Barani Afrika, njia za kukuza biashara baina ya nchi zao na uwekezaji katika sekta ya kilimo barani.
Chini ya kaulimbiu ya "Forging Inclusive Growth, Creating Jobs" viongozi pia watajadili kwa pamoja namna ya kukuza uchumi na uwekezaji kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Wakiwa Abuja viongozi pia watapata nafasi ya kujadili changamoto zinazolikabili Bara la Afrika zikiwemo za ukosefu wa ajira, matishio ya kiusalama, vikwazo vya usafiri barani, upungufu wa chakula na athari kadhaa za mazingira.
Akiwa mjini Abuja Rais Kikwete atakutana na viongozi kadhaa wa Afrika na Dunia kwa ujumla ambao wapo Abuja wakiwemo Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqian , Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu Bw. Gordon Brown ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza na viongozi kadhaa wa mashirika ya kiserikali na kibinafsi.
………………Mwisho………………
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
6 Mei, 2014
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe Daniel Ole Njoolay katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuriaMkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe Daniel Ole Njoolay baada ya kupokewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuriaMkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa baada ya kuwasili hotelini kwake na Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed baada ya kuwasili jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
PICHA: IKULU
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments