[wanabidii] Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania

Thursday, May 08, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Sefue, uteulzi huu umaanza tarehe 06 Mei, 2014.  Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba,2013.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.

Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-

    Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
    Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
    Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
    Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).

    Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
    Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.
    Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.

Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).

Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.

 "Mwisho"
Imetolewa na:

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
08 Mei, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments