[wanabidii] Ongezeko la matumizi na ukosefu wa kondom Singida na Rukwa

Monday, May 19, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

18 Mei, 2014
Hakikisha upatikanaji wa kondomu kuokoa maisha ya watu
Miongoni mwa watu wengi wana fikra potofu kuhusu matumizi ya kinga, upo ushaidi wa kutosha kuwa matumizi na uhitaji wa kondom umeongezeka katika vituo vya afya na vile vinavyotoa huduma za kijamii za kiafya vinashindwa kufikia uhitaji huo. Licha ya upungufu wa kondom za bure, zipo zile zinazouzwa na wauzaji huwa wana kondom za kutosha na wanamtandao mkubwa na vituo vya usambazaji nchi nzima. 

Wananchi hasa wanaoishi vijijni wanatakiwa kuacha utegemezi na kujifunza utamaduni wa kununua kondom ambazo zinauzwa kutoka kwa wauzaji kwa kinga zao wenyewe na wawapendao kwa kuwakinga na maambukizi ya magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa badala ya kusubiri kugawiwa kinga za bure kutoka vituo vya afya.

Taarifa kutoka mradi wa ushiriki sawa wa wanaume (TMEP) inaonyesha upungufu mkubwa wa kondom zaidi katika maeneo ya vijijini zaidi katika mkoa wa Rukwa na Singida. Upungufu katika maeneo haya umetokana na matumizi makubwa ya kondom kutokana na elimu inayotolewa na mradi wa TMEP unaohamasisha haki za afya na ujinsia(SRHR) kupitia shirika la HAPA na RODI ya mkoani Rukwa na Singida.

Takwimu katika mikoa hii miwili inaonyesha kuwa utekelezaji wa mradi huu wa TMEP umezaa matunda kutokana na ongezeko la uelewa juu ya haki ya afya na ujinsia SRHR na matumizi ya komdom, mimba mashuleni zimepungua mkoani Rukwa kutoka asilimia 86 mwaka 2012 hadi 50 mwaka 2013 na asilimia 62 mwaka 2012 hadi 33 mwaka 2013 mkoani Singida.

Utafiti pia unaonyesha kwamba shule zilizo na walimu na waelimishaji rika waliofundishwa (PEs) zimeonekana zikifanya vizuri katika kupunguza mimba ukilinganisha na shule ambazo zina mwalimu aliyefundishwa tu au muelimishaji rika tu. Shule ambazo hazina mwalimu aliyepewa mafunzo au mwanafunzi muelimishaji rika zina kiwango kikubwa cha mimba licha ya kuwa ndani ya eneo mradi unakoendeshwa. Kwa upande mwingine shule zilizo na walimu waliopewa mafunzo au mwanafunzi aliyepewa mafunzo ya uelimishaji rika wanamchango kiasi ingawa sio kama ilivyo katika shule zilizo na mwalimu na mwanafunzi waliopewa mafunzo.

Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa mradi wa TMEP umegundua kuwa, kutokana na ongezeko la uhitaji wa kondom, vituo vya afya vinagawa kondom kwa wale tu waliojiunga katika mpango wa uzazi wa mpango hao ndio wanaowatambua kama wateja wao, na wafanyakazi wa vituo hivi vya afya wahutoa taarifa inayoonyesha wapokeaji wa huduma hii, hivyo kuwawia vigumu kugawa kwa wale ambao hawajajiunga na mpango huu wa afya ya uzazi.

Hamis Maila, mratibu wa TMEP anasema kati ya watu 150 ambao wamepima afya zao mwaka (2013) kata ya Mgori mkoani Singida, mtu mmoja alikuwa ameambukiwa magonjwa ya ngono STI. "hii imetokana na matumizi ya kondom ambayo nilikuwa nawapa baada ya kuzipata katika mradi huu wa TMEP sasa upungufu wa kondom umekuwa tatizo na watu wengi wananiuliza 'Bwana kondom kwanini umetutenga?'"

Utafiti kwa upande mwingine umeonyesha kuwa sehemu zenye upatikanaji wa kondom katika vituo vya afya, watu wanatakiwa kujiandikisha katika mpango wa uzazi kwanza na wanaelimishwa njia salama za uzazi wa mpango kabla hawajapewa kondom. Mradi wa TMEP hivyobasi unahamasisha wanaume sio katika mikoa hii miwili ila nchi nzima kujiunga katika uzazi wa mpango sio kwa ajili ya kuwa na watoto wachache katika familia lakini pia kulinda afya ya wenza wao na familia kwa ujumla.

Kondom zinaumuhimu sana kwa wananchi kutokana na umuhimu wake katika kuzuia mimba zisizotarajiwa na kuenea kwa magonjwa ya ngono na UKIMWI. Hivyo basi kuna haja ya kuwa na vita isiyoisha dhidi ya magojwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa na kushinda vita hii.

Mradi wa TMEP pia unahamasiha wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhakikisha upatikanaji wa kondom kwa wanaohitaji kutoka vituo vya afya na kliniki zaidi katika maeneo ya vijijini ili kusaidia kuokoa maisha.

Imeandaliwa na:

Cuthbert Maendaenda,
Project Manager, TMEP Secretariat
RFSU Dar Office, 254 Manara Road, Ada Estate
P O Box 39806 Dar Es Salaam Tanzania

Tel: 255 222 668 930; Mobile +255 767 60 40 54; +255 786 35 45 05

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments