[wanabidii] LUGORA AMSUTA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI (CHIKAWE)

Friday, May 16, 2014
Lugora leo wakati anachangia hoja ya kupitisha bajeti ya wizara ya mambo ya ndani leo hii amemsuta Waziri wa mambo ya ndani LIVE huku waziri mwenyewe akionekana kwenye TV akiwa amefadhaika sana . Safi sana kama wabunge wote wangekuwa kama huyu Lugora tungefika mbali kimaisha Watanzania. Najua kuna baadhi ya wabunge pia ni wazuri kama huyu lakini walio wengi ni wale ambao wachumia tumbo wapo kwa  kuwafurahisha viongozi wao. Amesema inabidi waziri Chikawe aone aibu kwa kuleta bungeni bajeti isiyotekelezeka na isiyo na tija kwa wizara na kwa wananchi kwa jumla na sina hakika kama aliona aibu ya dhati maana hawa wenzetu hawaoni aibu. Sikujua kumbe bajeti iliyopita  zilitengwa fedha kwa ajili ya  ujenzi  wa nyumba za polisi maeneo mbali mbali lakini sehemu zingine fedha zilifika robo na  sehemu zingine hazikupelekwa kabisa. kama nilimsikia vizuri alisema Bukoba peke yake zilitengwa shilingi millioni 500 kwa ajili ya nyumba za polisi lakini haikufika hata senti tano. Bajeti hii zinaombwa fedha zingine kwa shughuli ile ile. Hivi watu wamefanya Bunge ni shamba la bibi msimu ukifika kwao ni wakati  wa mavuno kwa kuwadanganya wananchi halafu bajeti ikipita wamevuna mahela ya bure yanaingia mifukoni mwao.Mwaka mwingine wakati wa bunge ukifika wanaomba mihela mingine wabunge wanapitisha tu hata hawaulizi za mwaka jana zimefanya nini. Tunakwenda wapi? Sasa nimejua kumbe ndio maana wakati wa kupitisha bajeti mawaziri wanatoa hongo kubwa kwa wabunge ili bajeti zao zisikwame ili waneemeke. Nakumbuka wakati fulani wizara ya nishati na madini ilivyopitishwa kwa rushwa hadi ikaleta kizaazaa. Doh Wajinga ndio waliwao

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments