[wanabidii] BUNGE LA BAJETI LINA MVUTO?

Wednesday, May 21, 2014
Ndg zangu wanabidii
Nijuavyo mimi Kikao cha Bunge la Bajet ni muhimu kuliko kikao kingine chochote. Sababu ya msingi ni kwamba kikao hicho hutoa dira halisi ya kiuchumi na maendeleo ya Jamii. Lakini nimepata wasi wasi na kikao cha sasa kukosa mvuto na hata umuhimu. Mambo nyeti kama utalii, Elimu nk naona kama yanapita kienyeji bila msisitizo unaotakiwa.

Licha ya hayo, baadhi ya mawaziri na manaibu wao na wabunge wanajalli mambo ya siasa na vyama vyao zaidi kuliko kikao hicho cha Bunge. Mfano sidhani kama wabunge wa Tabora walikuwa bungeni Juma lililopita. Waliambatana zaidi na katibu mkuu wa chama Chao. Sasa amehamia mkoa mwingine. Nadhani atawasomba wote bungeni pia. Chadema nao hawako nyuma. Si tunawaona kwenye Runinga?

Katika hali hii nimepata wasiwasi mkubwa kama wanasiasa wa Tanzania ni kweli wana uchungu na nchi yao na wana nia thabiti ya kuleta maendeleao na maisha bora kwa watanzania. Wanajitahidi  kuingia madarakani kwa faida yao tu. Nakosa imani....
kessy

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments