[Mabadiliko] SABABU ZA CCM KUKATAA KATIBA MPYA

Tuesday, May 20, 2014

Kwa uchache, vifuatavyo ni vifungu vilivyomo katika sura mbalimbali za Rasimu ya Pili ya Katiba ambavyo ni vigumu kumeza kwa wanaCCM, hali iliyowafanya wavuruge zoezi la upatikanaji wa Katiba Mpya ili katiba ya zamani iendelee kutumika kwa manufaa yao. Kisingizio cha gharama za kuendesha Serikali 3 ni kiinimacho tu:
 
1.-(2) Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa zifuatazo:
(a)   utu;
(b)   uzalendo;
(c)    uadilifu;
(d)   umoja;
(e)    uwazi;
(f)    uwajibikaji; na
(g)   lugha ya Taifa.
 
SABABU:
Hizi tunu za Taifa ni mwiba mkali kwa CCM kwa kuwa hawana utu, uzalendo, umoja, uwazi wala uwajibikaji wowote. Hawana mpango wa kuzizingatia tunu hizi, ndio maana wanazipinga kwa nguvu zote ndani ya bunge la katiba huku watanzania wote tukiwasikiliza kwa mshangao mkubwa. Kila raia mwenye uchungu na nchi hii ameshikwa na bumbwazi kusikia kwamba CCM hawataki Tunu za Taifa. Hivi hawa CCM wanataka kutupeleka wapi jamani?
 
13.-(2) Dhamana ya uongozi na heshima kwa kiongozi wa umma itazingatia mambo yafuatayo:
(a)   uteuzi kwa misingi ya mwenendo wa mtu, uwezo, sifa, au uchaguzi uliyo huru na wa haki;
(b)   uwezo pasipo upendeleo katika kufanya uamuzi, na kuhakikisha kwamba uamuzi haufuati udugu, ukabila, udini, upendeleo, rushwa au ubaguzi wa aina yoyote.
 
SABABU:
  1. Kidonge hiki ni kichungu sana kwa CCM kumeza. Watanzania tunashuhudia jinsi serikali ya CCM inavyogawa vyeo kwa makada wake kama zawadi bila kuzingatia elimu, weledi, uwezo au sifa. Wakuu wa mikoa na wilaya huteuliwa tu kama njugu kwa makada au marafiki wa mwenye mamlaka ya uteuzi bila kuzingatia elimu au uwezo wa wahusika. Mara nyingi tumeona watu wa ajabuajabu, wasiokuwa na elimu na uzoefu wowote wakiteuliwa kushika vyeo hivi vya kifalme. Hali ni hiyo hiyo hata katika uteuzi wa watumishi wa umma kama vila makatibu wakuu, mawaziri, wakurugenzi, nk.
  2. Sote ni mashahidi jinsi serikali ya CCM ilivyojaa upendeleo, rushwa, ukabila, udini, na ubaguzi wa kila namna. Uteuzi wa viongozi wa umma katika nafasi mbalimbali za utumishi hutolewa kwa upendeleo na kwa itikadi za kidini, kikabila na hata kikanda. Kwa hiyo, CCM hawakipendi hiki kifungu kwa kuwa kinawabana wasifanye madudu katika ofisi za umma na kuteuana kishikaji katika kujaza nafasi za utumishi wa umma kama walivyozoea.
 
 
 
42.-(1) Kila mtu ana haki ya:
(a)   kupata fursa ya kupata elimu BORA bila ya vikwazo;
(b)   kupata elimu BORA ya MSINGI bila ya malipo na inayomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya ngazi inayofuata au kuweka msingi wa kuanza kujitegemea;
(c)    kupata elimu BORA inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu; na
(d)   kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ilimradi ana sifa stahiki za kupata elimu hiyo, bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
 
SABABU:
  1. CCM hawapendi kuona watanzania wakipata elimu BORA kwa kuwa wanafahamu fika kwamba wananchi wakielimika hawatatawalika. Kwa kuwa wanafahamu kwamba mtaji wao ni ujinga wa watanzania, hawako tayari kuwaelimisha kwani kufanya hivyo ni sawa na kunoa kisu ambacho kitawakata wao wenyewe. Badala ya kuboresha elimu, wako tayari kufungua shule za kata ambazo zinazalisha vilaza zaidi.
  2. Kwa kuwa haki hii itakuwa ni ya kikatiba itakuwa rashisi kwa wazazi ambao watoto wao hawajaelimishwa ipasavyo kufungua kesi mahakamani kuidai serikali fidia, jambo amabalo CCM hawataki hata kulisikia. Wanataka watu waendelee kueleimishwa chini ya kiwango, huku wakikwepa kuchukuliwa hatua kwa uzembe huo.
  3. CCM hawataki kuona wanafunzi wakisoma bure kwa sababu fedha ambazo zinatengwa kwa ajili ya elimu huliwa na mafisadi wa CCM bila ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Wahisani hutoa Tsh 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka lakini fedha hizo haziwafikii wanafunzi ila huishia kwenye matumbo mapana ya mafisadi wa CCM. Hili suala likiwa la kikatiba, CCM watashitakiwa kwa kushindwa kufikisha fedha hizo mashuleni, jambo ambalo wasingependa liwatokee.
 
 
101.-(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa Mawaziri au Naibu Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano:
 
(a)   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Jamhuri ya Tanganyika, Wajmbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar au madiwani katika Nchi Washirika.
(b)   Mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika.
 
SABABU:
  1. Wabunge wa CCM wamezoea kuteuliwa kuwa mawaziri hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutafuna rasilimali za taifa bila kunawa. Hawawezi kukubali waukose uwaziri kwani kwao uwaziri sio utumishi bali ni ulaji na utapanyaji wa mali za umma na rasilimali za taifa.
  2. Watu wengi wa CCM ni mafisadi. Kamwe hawakipendi kifungu hiki kwani wengi wao watakosa vyeo endapo katiba mpya itapita na karibu wote wataishia Segerea. Wangependa tuendelee na katiba iliyopo ambayo haina meno ya kuwabana mafisadi na wabadhirifu wa mali za wananchi.
 
125.-(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuteuliwa kuwa mbunge ikiwa:
(a)   mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka 5
 
SABABU:
  1. CCM hawapendi kuwepo na ukomo wa ubunge kwa kuwa wanadhani kwamba wao walizaliwa kwa ajili ya kutawala.
  2. Kuwa mbunge kunawawezesha CCM kuteuliwa kuwa mawaziri hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kufanya ufisadi na kutafuna mali za umma. Na kwa vile CCM ni mafisadi wa kutupwa hawataki kabisa kupoteza fursa hii adhimu ya kuendelea na ufisadi wao wa jadi.
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments