Kuna post ambayo Bariki Mwasaga alituma jukwaani kuhusu muhtasari wa kikao cha UKAWA kama ambavyo ilirushwa Wanabidii na baada ya kuirusha kwenye jukwaa Makene kama msemaji wa Chadema alitoa taarifa kamili juu ya uvumi huo. Vilevile Mtatiro kwa upande wa CUF naye alieleza jukwaani kuhusu hoja hiyo hiyo. kwa bahati mbaya sipati muda wa kufuatilia michango yote kwa wakati lakini ninapopata fursa nafuatilia michango yote hata kama muda umepita. Dhumuni langu nikujenga jukwaa linaloweza kuvumiliana na kujenga hoja kwa hekima na busara hasa ukizingatia wote nia yetu ni moja nayo ni kupashana habari, kuelimishana, kukosoana na kushauriana.
Jambo la kusikitisha kabisa Gikaro usiku wa manane kachangia kwa lugha ya maudhi isiyopendeza kwa mtu yeyote ambaye wote tunafahamu kuwa anazo akili timamu na kwa kuweka taarifa jukwaani hakuna kosa lolote alilolifanya.
Mchango wake ni huu hapa chini,
" Please Moderators, kwanini mnaruhusu vichaa wanaposti ujinga kama huu hapa jukwaani pasipo kufuta posti hii na kuwafungia wahusika? Mtasababisha hili jukwaa lionekane la kihuni."
Lugha hii siyo ya staha hata kidogo, Binafsi naamini na najua weng wanaamini kuwa Bariki Mwasaga anayo akili timamu na ufahamu wa kutosha katika masuala mbali mbali. Kama haitoshi, humu jukwaani hajawahi kumdharau mtu au kumtukana mtu hata pale aliposhambuliwa moja kwa moja kwa lugha kali na kebehi.
Ninakutaka Erick Gikaro kwa muda wako uliombe radhi jukwaa hili kwa matumizi mabaya ya lugha na kusababisha maudhi na mauvimu kwa baadhi ya watu waliosoma ujumbe huu.
Ahsante
_________________________________________________
Nicomedes M. Kajungu
P.O.Box 7733, Mwanza.
Nicomedes M. Kajungu
P.O.Box 7733, Mwanza.
+255 782 315 688, +255 767 48 32 71,
+255 719 451 850
Skype add: nkajungu
Skype add: nkajungu
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAJsbJR0Mx9pXGz6EZoLuJWDCPxyAYUGfx%3DeSNV7UKe4u-DbTPA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments