Ndugu Wazalendo
Leo nimeamua kuwafikishia hoja hii katika mchakato huu wa katiba, ambao walopata fursa kuingia katika bunge hilo, tunawaomba walifikirie kwa kina suala hili la ulinzi na usalama kuwepo katika oroza ya mambo ya muungano, tunatakiwa tuangalie faida na hasara katika taifa letu.
Niaze na hasara
Kwanza kitu cha kwanzo ambacho kinanitatiza ni suala la uwanifu baina ya pande mbili za muungano, hasa wenzetu ambao ni watanganyika, hawajawahi kuwafanyia mema wazanzibari toka kuanzishwa kwa muungano huu, ni kudhalilishwa na vikosi vya muungano, Jeshi la ulinzi JWTZ na Police.
Kutokana na mfumo wa sasa ulio pendekezwa, katika sura ya SABA mamlaka ya rais wa muungano.
kifungu 71.2 Rais wa jamuhuri wa muungano atakuwa mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu.
kifungu hiki kifutwe, Na badala yake kisomeke hivi.
Rais wa Jamuhuri wa muungano atakuwa mtendaji na mtekelezaji mkuu wa vikosi vya ulinzi kwa mujibu wa makubaliano wa viongozi wawili ambao ni Rais wa Zanzibar na Tanganyika.
Nasema hivi ili kupunguza madaraka ya rais wa muuungano, kwa sababu anaweza kushawishika na uroho wa madaraka na kuyatumia vibaya madaraka hayo bila ya kuwashirikisha marais wa pande mbili za muungano.
Pili Rais wa muungano anaweza akayaamuru majeshi na kupindua nchi pande yoyote ya muungano, iwe Tanganyika au zanzibar au serikali zote mbili kupinguliwa, hivyo basi Rais wa zanzibar ndio anatakiwa Awe amiri jeshi mkuu na kiongozi kwa majeshi yote yalioko zanzibar, na Tanganyika vile vile kwa majeshi yote yalioko Tanganyika. Rais wa muungano asiwe na mamlaka ya kuamrisha chochote mpaka apate idhini ya marais hawa.
Jengine ambalo ni muhimu zaidi, muundo wa jeshi, kwa sasa muundo wa jeshi la ulinzi, naweza kusema watanganyika wamechukua asilimia 99 za uwajiri, mpaka waliko zanzibar wote ni watanganyika, kiasi ambacho wazanzibari wanaona kama vile sisi tumekuwa koloni la tanganyika.
Hivyo basi katika mfumo mpya wa muungano, Kama suala hili litakuwepo katika muungano, ushauri wangu ni kwamba.
Kwanza majeshi yote yatakayo kuwepo zanzibar ambayo ya muungano wawe wazanzibari wenyewe tu, sio kama mfumo wa sasa kuletewa watanganyika, sisi tuko 1.2 Milioni, jeshi la watu 3000 uwekano upo wa kupatikana vijana wa kizanzibari, hivyo basi nasi tutafaidika katika mfumo huu wa muungano katika ajira, na police hivyo hivyo wazanzibari wenyewe. Na rais wa zanzibar ndio atayaongoza majeshi yote yalioko zanzibar kama amiri jeshi mkuu wa nchi.
Hii itaondoa zana ya kwamba wazanzibari tunatawaliwa, na pia tutapunguza gaharama za muungano, kwa mfano hivi sasa wale watanganyika walio letwa zanzibar, serikali inawaagharamia makazi na chakula. hivyo kama tutaajiriwa wazanzibari wenyewe, gharama hizo hazitakuwepo kwani sisi hapa ni kwetu, gharama hizo tutazibeba wenyewe.
Hebu tuangalie mifano nchi za wenzetu katika suala la ulinzi.
Kwa mfano NATO, ambalo ni barazala usalama ulaya,nchi zote zilizo jiunga katika Nato, pale panapohitajika jeshi baada ya maamuzi ya makubaliano na nchi hizo zimeungano kila nchi hutoa wananjeshi wake kuchangia katika vita au kwenda kueka usalama ambako waliko kusudia,hivyo basi ingawa suala la usalama limekuwa la muungano wa pamoja lakini kila nchi ina majeshi yake, na inajilinda wenyewe bila ya kulindwa na mtu kama vile tunavyo fanyiwa sisi wazanzibari kuletewa wananjeshi kutoka bara.
Na kila wakati wa uchaguzi hutuletewa maelfu wa wanajeshi na vifaru kututisha kwa ajili ya mapinduzi ya kura, hivyo basi hatua hii ifikie kikomo. Tumechoka kudhalilishwa na Muungano na Viongozi wa Tanganyika ambao hutumia muungano kwa manufaa yao.
Wametuuwa 1964 katika mapinduzi, wametuuwa 1995 katika uchaguzi mkuu, wametuuwa 2001, 2005, vyote hivyo ni vikosi vya muungano na amiri jeshi kuu wao ni Rais wa muungano , basi tena mutatumalizaaaaa.
Nawakilisha hoja.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments