Nachukua nafasi hii kutoa maoni yangu kama Mtanzania ninaeamini kuwa umoja, amani, utulivu na mshikamano tulionao ni matunda ya kazi nzuri iliyofanywa na waasisi wa Taifa letu la Tanzania.
Waasisi hao kwa nyakati mbali mbali wametuasa kuwa kuunda serikali ya Tanganyika kutapelekea kuvunja Muungano wetu na pia kutatengeneza dhambi kubwa ya ubaguzi dhidi ya wengine.
Dhambi hii ukishaiifanya ni vugumu kuachana nayo, maana kuna kundi fulani la watu toka sehemu fulani watajioni ni bora kuliko wenzao wanaotoka sehemu nyingine. Tutaanza kujitambulisha kwa maeneo tunayotoka mfano wa kanda ya ziwa, wa kanda ya pwani, Unguja, Pemba n.k hivi Watanzania wa leo tunataka kufikia huko ? Kama leo kuna watu wanjiona wao ni Watanganyika kwa nini baadae wasiojione wao ni wakaskazini au kusini n.k. Mwalimu walituasa kuwa nje ya Muungano hakuna Zanzibar wala Tanganyika, Nje ya Muungano kuna wale Wapemba na hawa Waunguja, nje ya Muungano hakuna Tanganyika kuna hawa wabara na hao na wa pwani, tusijidanyanye kuwa tukiunda Tanganyika tutabaki salama sio kweli, Muungano utavunjika na kila kanda itatataka kujitambua na kuunda serikali yake na kujiamulia mambo yake, ndugu zangu hapo tutakuwa salama ?
Tuangalie mifano ya Mataifa makubwa yaliyojaribu kuunda serikali zao mf. Russia walipounda Serikali yao ndani ua USSR hapo ndio ulikuwa mwisho wa Taifa hilo kubwa duniani, zipo nchi zina Muungano kama wetu mf. UK wana Serikali ya Muungano wa nchi 4 serikali 4 na sio 5, yaani Scotland, Wales na Northern Ireland kila mmoja ana Serikali yake kwa sababu ni nchi ndogo katika Muungano wa UK ila England kwa sababu ni nchi kubwa katika Muungano ule madaraka yake yote yako kwenye Serikali ya Muungano, sasa hapa kwetu tatizo ni nini ?
Kama tatizo ni Zanzibar kuwa na bendera, wimbo na Rais mbona hata timu za mpira zina MaRais, nyimbo zao na bendera zao ? Mbona katika miungano mingine mf. USA kila jimbo lina bendera, wimbo na Gavana wake Je hiyo inaondoa Utaifa wao kwa USA ? Zanzibar ni nchi ndogo katika Muungano hivyo ni muhimu kupata upendeleo zaidi katika Muungano ili isonekane imemezwa na nchi kubwa Tanzania bara, mifano iko mingi kama UK, China na Hongkong n.k
Ndugu zangu ukiacha maelezo hayo tufikirie gharama za uendeshaji wa Serikali ya 3 na taasisi zake, Je tutaweza kweli kuondoa umasikini, ujinga na maradhi ?
Katika historia ya dunia hakuna Taifa lolote lililoamua kuunda serikali za nchi(majimbo) yenye nguvu au makubwa ndani ya nchi na likabaki salama mf. USSR, Yugoslavia n.k
Kwa wale tunaodai serikali ya Tanganyika labda tuna malengo mengine zaidi ya malengo makuu yanayojionyesha wazi wazi.
Lakini kwa hoja wale wanaodai serikali 3 hawana zaidi ya kutumia rejea za watu ambao wengi wao sasa hivi ukiwauliza bado wanaamini muundo wa Serikali 2 ndio bora, mf. Prof. Shivji, ambae naona amefanyiwa marejeo kadhaa na baadhi ya watoa hoja kwenye Bunge la Katiba.
Kama kweli tunataka kuendelea na Muungano wetu ni dhahiri shahiri hatuna haja ya kuunda serikali ya 3 badala yake turekebishe kasoro zilizojitokeza ili tuimarishe Muungano wetu.
Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanaotaka kutagawa washindwe na walegee.
Phares Magesa
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments