RED BRIGADE WAMPIGA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE (CHADEMA) TAIFA!
Vijana wa Red Brigade leo wamevamia mkutano wa viongozi wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini na kuwapiga wajumbe wa mkutano huo na kuwajeruhi vibaya Mwenyekiti wa Baraza la wazee Taifa Ndg Nyangaki Shilungushela pamoja na mjumbe mwingine ndg Mariam Philipo!
Mzee Shilungushela ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kambarage mjini hapa amejeruhiwa usoni baada ya kupigwa vichwa na RED BRIGADE hao!
Hali ni mbaya zaidi kwa Bi Mariam Philipo ambaye amepigwa na kuvunjiwa miwani yake na vioo vya miwani hiyo kumwingia kwenye jicho lake la kushoto!
Tukio hili tayari limesharipotiwa polisi limechukua sura mpya mjini hapa kutokana na viongozi kulipoti suala hilo kwa Latino mkuu Dr Slaa huku viongozi wengine wakisema kuwa vijana hao wapo nyuma ya Dr Slaa hivyo hakuna kitakachofanyika kwao!
Hadi sasa hali za viongozi hawa si nzuri na tukio hili ni la pili baada ya Red Brigade kuwafungia ndani baadhi ya viongozi wasishiriki mikutano ya chama!
Kitendo hiki kimezidi kuchochea wasi wasi walionao wakazi wa shinyanga juu ya chama hiki! Mmoja ya watu waliokuwepo eneo hili alisema wazi kuwa amepoteza imani na chama hiki!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments