[wanabidii] Mipasho ya bunge maalumu la katiba tarehe 14 Aprili 2014

Monday, April 14, 2014
Haya ni maneno yaliyosemwa na baadhi ya wajumbe wa bunge maalumu la katiba leo tarehe 14 Aprili 2014.

Tanganyika ikirudi itazaa jamhuri ya Makonde, Nyamwezi!

Mbona Comoros haijawa Hong Kong?

Unadai cheti cha kuzaliwa cha baba yako ili iweje?

Mtu anayefanya mambo kipekeyake anaitwa mchawi!

Nyerere alikufa akiwa mwana CCM na alikufa akiwa ahajabadili msimamo wake, lakini alifariki baada ya tume zote kufanya mambo yake!

Kero za muungano zitamalizwa na taratibu mtakazoziweka....na mkishindwa kusikilizana wageukieni viongozi wa dini, mfano, Pengo alisema Serikali mbili zinatosha!

Tunaomba rasirimali zirudi mikononi mwa wananchi.

Kaa kitako, mjinga tu (imesikika kwa pembeni).

Zanzibar ni nchi na JK anajua hilo. Ndiyo maana alipoenda kwenye sherehe za mapinduzi alikaa na akamsubiri mwenye nchi. Na katika kuondoka aliondoka kwanza Rais wa wa Znzibar mwenye nchi.

Hamna lolote...mnaogopa gharama nyie kweli? Mbona mmeweka mawaziri mpaka wasio na wizara maalumu?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments