WAKATI RWANDA IKIADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MIAKA ISHIRINI BAADA YA MAUAJI YA KIMBARI TUNAHITAJI KUJIFUNZA
Rwanda wameadhimisha leo miaka ishirini baada ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994, Nawapa pole wananchi wote wa Rwanda kwa namna walivyoathirika na tukio lile baya pengine kuliko yote kuwahi kutokea kwenye ukanda huu wa Afrika,
Cha kusikitisha ni kwamba madhimisho haya yanafanyika huku jumuiya yea kimataifa ikiwa haijachukua tahadhari ya kutosha kuhakikisha maafa kama yale hayatokei tena, tazama yanayoendelea Afrika ya kati.
Nasema haya kwa sababu kumbukumbu zinaonyesha kua kwenye mauaji ya kimbari ya Rwanda Jumuia za kimataifa zilistahili kulaumiwa na na zitaendelea kulaumiwa kwa Uzembe wa makusudi, kwani tahadhari zilitolewa napema sana na wataalam mbalimbali kuhusu Uwezekano wa kutokea maafa lakini hakuna hatua zozote za haraka zilizo chukuliwa mpaka mauaji yale yakatokea,
Hata sasa kile kinachoendelea Afrika ya kati na maeneo mengine tahadhari ingechukuliwa mapema pengine hali isingekua mbaya kiasi ilivyo sasa imekua ni kawaida kwa jumuiya za kimataifa hasa UN kujivuta sana na kusubiri hadi hali iwe mbaya ndio waseme wanafanya "humantarian intervention", Hakika hatuwezi kulinda amani na kujihakikishia usalama wa dunia kwa mfumo huu.
Niipongeze serikali ya Rwanda vilevile kwa hatua za makusudi walizochukua kuhakikisha kuwa tukio kama lile halijirudii tena, najua si jambo rahisi kwa jamii zenye makovu ya aina hii kusameheana lakini mfumo uliobuniwa wa kutumia mahakama za kitamaduni maarufu kama "Gacaca court" umesaidia kwa kiwango kikubwa kuziunganisha jamii hizi mbili hasimu ( Wahutu na watusi ), vilevile serikali ya Rwanda kupiga marufuku vitendo vya kuendekeza ukabila ikiwa ni pamoja na kuzuia mtu yeyote kujitambulisha au kumtambua mtu mwingine kwa jina la kabila lake ( kufanya hivyo ni kosa la jina) imesaidia kwa kiwango fulani kuzuia "ethinic politicization"
Tanzania na sisi tumeanza kuonyesha dalili za kuelekea huko sijui kwanini tunashindwa kujifunza kupitia jirani zetu hawa Rwanda na Kenya, Hivi hatuwezi kufanYa siasa bila kuwagawa wananchi katika misingi ya Dini, Kanda na Ukabila?
Tujisahihishe
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments