Kesho, Jumamosi Aprili 19, 2014 Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamepanga kufanya mkutano wa hadhara Zanzibar kwa malengo ya kuongea na wananchi juu ya msimano wao wa kususia vikao vya Bunge.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma, mwakilishi wa kundi hilo Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa katika kikao chao wamekubaliana kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kwa
wananchi kwa kuwajumuisha wajumbe wasiokuwa na dharura.
"Tumekubaliana kwamba siku ya Jumamosi kwa pamoja Wabunge wote ambao hatuna dharura tukuwa tumeenda Zanzibar, kutakuwa na mkutano wa hadhara kuanzia saa nne asubuhi. Tutaondoka na siku hiyo na Boti ya saa moja asubuhi kuelekea Zanzibar. Katika mkutano wa Zanzibar tutaeleza yaliyojiri katika Bunge hili Maalumu...." alisema Lipumba kama anavyosikika kwenye video iliyopachikwa hapo chini.
Viongozi wa Ukawa walotoka nje ya Bunge Maalum jana wakipinga jinsi mjadala wa Katiba Mpya unavyokwenda, na kudai kuwa hawako tayari kurudi Bungeni humo wiki ijayo, wala hawatarejea kwenye kikao cha Agosti, endapo hawatahakikishiwa kuwa maudhui yaliyomo ndani ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya yatajadiliwa kama yalivyo.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta amesema anawasihi Wajumbe hao warejee katika Kamati ya Uongozi ili waeleze hatima ya uamuzi wao kwa maana una athari kisheria na kiutawala.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments