[Mabadiliko] NIMEBADILI MSIMAMO MUUNDO WA MUUNGANO

Friday, April 11, 2014

Bandugu nimekuwa muumini wa serikali mbili. Maoni yangu hayo yalitokana na maono yangu kuwa unapoungana unakuwa kitu kimoja. Hata sasa maoni yangu ni muungano wa serikali moja.
  Kwa hali ilivyo yaonekana hili jambo ni gumu.naamini ugumu wake unatokana na uroho wa madaraka wa wanasiasa.
  Sasa nimekuwa nikisoma sana hoja za pande mbili; pro tatu Vs mbili.kwa kweli kwa uchambuzi wangu naona hoja za upande wa tatu zinakuwa nzito na ushawishi.
  Nimesikiliza hotuba za bungeni jana. Hotuba ya kafulila ilinifanya nitafakari upya msimamo wangu. Lakini hoja za Habib mnyaa zimenilainisha kabisa.
  Sasa naamini Nyumba ya muungano ilijengwa kinyume na ramani kwenye makubaliano ya muungano. Kulikuwa na utofauti kwenye implementation. Kama hatuwezi kwenda moja, basi turudi kwenye kilichokusudiwa awali. Serikali tatu.
  Hata hivyo bado Nina hofu kuwa serikali tatu itavunja muungano.sasa hii ni hofu tu,na hisia.sasa ninalazimika kufuata matakwa ya kiakili badala ya hofu ambazo ni hisia.
  Nimesikiliza kongamano la juzi la bwawani Zanzibar.kwa kuwa zbar wanakubali tatu, basi ni heri kufa kesho kuliko Leo.
  Haya ni maoni yangu .naendelea kufatilia hoja.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6QidfnnUXgvNRG%3Di-F3jhdfcD0C0KhtMRKacYu8ZVFy2gw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments