[Mabadiliko] DHAMBI YA UBAGUZI INAWATAFUNA CCM!

Sunday, April 20, 2014
Kuna mbunge mmoja alisikika siku za karibuni akitoa kauli za kibaguzi na kichochezi katika bunge la katiba (BMK) na kushangiliwa sana na wabunge wa CCM. Nilishangaa sana kuona wabunge wenye akili zilizotimia wakishabikia dhambi hii ya ubaguzi. Huyu ni mbunge wa CCM kutoka upande wa Zanzibar. Alisikika waziwazi akisema kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika katika kisiwa cha Unguja na kwamba kule Pemba ilipelekwa bendera tu. Hakuishia hapo tu—aliendelea kuapa kwamba wale wasiotaka Muungano wa serikali mbili warudi "kwao". Aliendelea zaidi kudai kwamba hati ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar imepatikana, sasa hao watu (Wapemba) aliowataka warudi kwao (Uarabuni) sasa waanze kudai hati ya Unguja na Pemba. Na safari zote alipokuwa akitamka maneno haya alikuwa akishangiliwa kwa nguvu  sana na wanaCCM wenzake!
 
Kauli za chuki na za kibaguzi kama hizi sio za kushangilia wala kushabikia hata kidogo. Inakuwaje wana-CCM wamshangilie mtu anayetaka kubomoa umoja na mshikamano wetu badala ya kumkemea eti kwa sababu ni "mwenzao" na kwa kigezo kwamba wao ndio wanaotawala na hakuna mtu wa kuwahoji? Nchi hii ikimwaga damu kwa sababu ya kauli za kiintarahamwe kama hizi ni nani atakyebaki salama? CCM mnapaswa wakati mwingine kujifunza kutumia akili badala ya kutumia viungo tofauti na ubongo. Mmepewa akili mzitumie kuchanganua mambo sio kufugia nywele!
 
Sasa endeleeni kuchezea amani, siku likibumbuluka msitafute mtu wa kumlaumu. Hatuwezi kuvumilia kuona wajinga wachache wakiitumbukiza nchi katika vita huku tukiwa tumekaa kimya. Ni wazi vita ikitokea ktk nchi hii watakaoathirika ni wananchi masikini wasiokuwa na uwezo wa kuikimbia nchi. Watu wa CCM mmeishavuna pesa za kutosha kupitia kwenye ufidsadi. Ikitokea vita mtapanda ndege na kukimbilia nje ya nchi. Mistake kupalilia chokochoko ambazo zitakuja kugharimu maisha ya walalahoi huku watoto wenu mkiwatorosha kwenda nje ya Tanzania.
 
Tafakari, chukua hatua!

Share this :

Related Posts

0 Comments