[wanabidii] SERIKALI ITOE TAMKO KUHUSU WALIOKAMATWA KATIKA JARIBIO LA KUMUUA GEN NYAMWASA

Saturday, March 08, 2014
SERIKALI ITOE TAMKO KUHUSU WATANZANIA 3 WALIOKAMATWA KATIKA JARIBIO LA KUMUUA GEN NYAMWASA 

Ndugu zangu ,

Hali kati ya Afrika Kusini na Rwanda imekuwa si shwari tena baada ya watu kujaribu kumuuwa mkuu wa zamani wa majeshi ya rwanda aliyepo hifadhini nchini afrika kusini .

Huyu mkuu anaitwa Nyamwasa , wakati watu hao wanavamia hakuwepo kwahiyo hiyo ndio ilikuwa salama yake , kabla ya tukio hili kuna matukio mengine yameshawahi kufanywa ya kujaribu kumuuwa .

Vyombo vya usalama vya afrika kusini vumeshakamata watu 6 ambapo 3 ni raia wa rwanda na 3 ni raia wa Tanzania , lakini serikali ya tanzania kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa bado haijatoa taarifa wala tamko lolote kuhusu watanzania hawa .

Ukumbukwe pia miezi kadhaa iliyopita magazeti ya rwanda yaliwahi kuandika habari zinazotuhumu serikali ya tanzania kukutana na viongozi wa waasi na kuwapa hati za kusafiria za Tanzania .

Inawezekana mpango wa Rwanda ulikuwa ni kutengeneza suala hili la hati ili waje kufanya shambulio hili dhidi ya Gen Nyamwasa na ionekana Kwamba Tanzania inahusika au ina mkono wake .

Tunaomba serikali  yetu kupitia msemaji wake au wizara husika kutoa Taarifa kwa umma kuhusu watanzania hawa waliokamatwa huko afrika kusini kama kweli ni raia halali wa nchi yetu au la .

Pia tunaomba serikali kuhakikisha inapitia upya utaratibu wa utoaji wa hati za kusafiria kwa siku zijazo na hili suala lisijirudie mara kwa mara .


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments