[wanabidii] Pandu Ameir Kificho - Sioni sababu ya kuwa na Serikali 3

Wednesday, March 19, 2014
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi na aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa
Bunge maalum la katiba Pandu Ameir Kificho amesema haoni sababu za
kuvunja muungano uliodumu miaka 50 sasa .

Pia alisema katiba mpya inakuja kwa lengo la kuimarisha muungano.
Kificho alisema hayo jana wakati wa mahojiano Mjini hapa na kubainisha
kuwa japo kuna changamoto lakini isiwe sababu za kuvunja muungano
kwani hata kwa upande wa Zanzibar wako waliotaka serikali ya mkataba,
wengine wakikata serikali mbili na tatu.

"Rasimu yote ililenga katika serikali tatu, suala la muungano kwenye
baraza la wawakilishi lilifika lakini hakukuwa na majibu ya moja kwa
moja" alisema.

Alisema muungano umedumu kwa miaka 50 lakini hata wazo la Rais JakayaKikwete wa Tanzania na Rais wa Zanzibar Dk.Ally Mohamed Shein nia yao ya kutafuta katiba mpya ni kuimarisha muungano.

Kificho alisema kuna haja ya Wananchi kushikamana ili kufanya muungano
kuwa bora zaidi.

"Sasa inapendekezwa serikali ya tatu, serikali ya juu yenye kuelea
elea hapo kuna hatari ya kuanguka" alisema.

Alisema msimamo wake ni serikali mbili na utaratibu unaofaa ni wa
serikali mbili.

Pamoja na hayo alisema utayarishaji wa kanuni ulikuwa na changamoto
nyingi na ulitakiwa uvumilivu wa hali ya juu ili kuweza kutoa maamuzi
sahihi.

Kificho ambaye alikuwa mwenyekiti wa muda wa bunge maalum la katiba
alisema amekuwa akipokea pongezi kutoka maeneo mbalimbali za
kumpongeza kwa kufanikisha kazi ya kuandaa kanunui ambayo ilikuwa na
changamoto nyingi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments