[wanabidii] MUUNGANO WETU NI WA KUIGWA AFRIKA

Friday, March 07, 2014
( Na Jovina Bujulu ,MAELEZO DODOMA)
Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni jambo la kujivunia kwa watanzania wote na katika bara la Afrika.

Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai wakati wa mahojiano katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC ONE.

Mh. Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa jambo la Muhimu tunalotakiwa kufanya kwa sasa ni kuimarisha na kuboresha Muungano ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo.

"Hatuna budi kuendelea kuuimarisha muungano uliopo ikiwa ni kichocheo cha maendeleo, tumeona mifano kwenye nchi kadha wa kadha zilizo katika muungano mfano nchi Marekani imekuwa mfano bora duniani kimaendeleo hasa kutokana na Muungano uliopo" Alisema Ndugai.

Mh. Ndugai aliongeza kuwa hata Muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akitukumbusha mara kwa mara kuusimamia muungano wa Tanzania na kuudumisha.

"Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiasa Watanzania wote kuudumisha Muungano wa Tanzania na kuepuka viashiria vyote vinavyoonekana kuvunja muungano, hivyo tushikamane katika kuudumisha". Alisema Ndugai.

Naye Mjumbe wa Bunge hilo ambaye mjumbe wa secretariati ya marekebisho kanuni za Bunge Maalum Mhesh. Evod Mmanda alisema kwamba miaka 50 ya muungano ni faraja na jambo la kujivunia.

"hatuna budi kwa pamoja kukaa na kuufikiria zaidi Muungano na kutatua changamoto zote zinazojitokeza ili kuudumisha muungano huu na Wasiopenda Muungano hawana sababu za kutosha" Alisema Mh. Mmanda.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments