[wanabidii] KURA YA WAZI AU SIRI ?

Wednesday, March 05, 2014
Mchakato huu ni wa kitaifa, kwa maana unawagusa watanzania. Rasimu inayojadiliwa kinadharia inatokana na wao. Wajumbe waliochaguliwa kuwawakilisha wanatokana na wao. Wangependa maoni na mawazo ya wajumbe wa bunge yatokane na wao. 

Katika muktadha huo wangependa kuwa na democratic faith dhidi ya wajumbe wao. Democratic faith haijengwi kizani. Democratic faith haijengwi mafichoni bali hujengwa hadharani na mbele ya macho ya wengi. Kura iwe wazi. Hili ni moja.

Pili wanafalsafa wanasema binaadamu kwa asili yake ni mbinafsi. Ili kuepuka ubinafsi wa mwanadamu katika muktadha unaogusa maslahi ya wengi unatafutwa mfumo ambao uta neutralize matakwa binafsi ya mwanadamu na hatimaye tunamvisha kilemba cha matakwa ya wengi. Kura ya wazi ni kilemba sahihi.

Tatu, hoja inayotumika kuhalalisha kura ya wazi ni hoja nyepesi. Vitisho na hofu katika historia ya demokrasia duniani havijawahi kutumika kuwa nyenzo za kuhalalisha maamuzi yanayogusa maslahi ya Taifa. Hoja zinazotumika ni uwezo wa methodolojia katika kukidhi matakwa ya wengi lakini siyo hatari ya methodolojia kutoa mwanya kwa wawakilishi kutishwa na vyama vyao. Kwa maana hiyo wanaohalalisha kura ya siri wamekosa msingi wa hoja yao.

Hata hivyo kiwango cha uwazi kiwe hivi.

Katika kupitisha kifungu kwa kifungu cha rasimu itumike kura ya wazi kwa sababu inagusa maeneo mahsusi ambayo kwa kiasi kikubwa kilemba cha matakwa ya wengi kinahitajika zaidi na wanye mchakato (watanzania) wangependa kuona ni jinsi gani matakwa yao yanawasilishwa.

Baada ya mchakato huo, katika kupitisha rasimu ya mwisho basi kura ya siri itumike kwani itakua tayari kila kipengele kimepitishwa katika mfumo wa wazi ambapo ubinafsi ulizikwa. Hivyo kama watavyofanya watanzania katika kura ya maoni basi ifanyike hivyo kuanzia bungeni kwa uwingi wa kura kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments