[Mabadiliko] Natafakari Katiba Na Ngamia...!

Wednesday, March 26, 2014


Ndugu zangu,

Kila kunapokucha, na kila ninavyotafakari kinachowasilishwa kwetu kupitia media kuhusiana na mchakato wa Katiba, nakiona kilichoandikwa kwenye vitabu vitakatifu, kuwa inawezekana kwa ngamia kupita kwenye tundu ya sindano, lakini si kwa tajiri kufika kwenye ufalme wa mbingu.

Imefika mahali ni kama vile tunatafuta tusichokijua, tena gizani na tumetanguliza mikono yetu.

Leo Wabunge wetu wametimiza siku 36 za kuwapo kwao Dodoma. Ni zaidi ya nusu ya siku 70 walizopangiwa. Na hawajavigusa vifungu vya rasimu ya Katiba. Ndio, hawajaianza hata sura ya kwanza ya Rasimu ya Katiba. Na bado tunaona Mwenyekiti akitumia muda mchache uliobaki kusimama na kuwatambulisha wageni wa wajumbe! Si ni wageni wa wajumbe, nani amesema ni wageni wa Bunge Maalum La Katiba?!

Lakini, mafanikio makubwa waliyoyapata wabunge wetu hadi sasa ni kujigawa katika mafungu makubwa na madogo. Tena kwa nderemo na kugonga meza. Kila kundi linatafuta chake, pengine si kile walichotumwa wakitafute. Na tena wamejikita katika Serikali na Muundo wa Muungano tu wakati kuna mengine mengi ya msingi na yenye maslahi kwa umma yanafunikwa.

Na katika nchi zetu hizi, ukiona Katiba inapatikana kwa misingi ya ' dhahania' kwa maana ya kusikia inatamkwa na Mwenyekiti; " Nadhani waliosema ' Ndiyo' wameshinda!" Basi, ujue pia hapo kuna tatizo. Kwamba inatosha tu kwa mwenyekiti ' kudhani'!

Naam, kwenye kabati langu niliiweka Katiba ya Mwaka 1977 inayotumika sasa. IIlishaanza kukusanya vumbi. Lakini, kwa vile kule Dodoma hatutafuti Katiba ya Mpito, na Katiba ya miaka 50 ijayo inaonekana ni ngumu zaidi, bali ya mwaka 2015 na labda na ya uchaguzi unaofuata, basi, nimeamua kuingia kabatini na kuichukua tena Katiba yangu ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1984. Nimeifutafuta vumbi tu na sasa iko karibu nami.

Na kwenye Sura ya Kwanza kabisa kifungu cha kwanza inasema;

"Tanzania ni Nchi Moja na ni Jamhuri ya Muungano."

Na kifungu cha 2(1) kinasema;" Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo."- Katiba JMT, 1977)

Naam, mimi naiona haja ya kuendelea kutafakari Katiba na ngamia...!

Ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7AUK16qQxLaLYVTAbFRna7err3odYkunYfayGfHwZD7g%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments