[Mabadiliko] MATAPELI WA NJIA YA SIMU MAKAMPUNI YANATUSAIDIAJE?

Wednesday, March 05, 2014

Huu ni ujumbe wa simu nilioupokea leo hii kutoka kwenye namba ya tapeli hii hapa 0688105449


“Habari za kazi bwana mdogo, naomba umrushie kijana wangu elfu 40 kwa mpesa kupitia namba 0753652854, nitakutumia baadaye huku mtandao unasumbua, ukifanikisha nitaarifu kupitia simu hii, simu haina chaji, JINA LAKE (Jina la kaka yangu)”.


Nilipoupokea ujumbe huu sikuwa nashaka kwamba aliyetuma ni kaka yangu maana jina pale mwisho ni la kaka yangu na ninajua ana mwanae anasoma chuo. Ilikuwa imeshapita kama nusu saa tangu sms iingie hadi naisoma, nikaona ni vema nimpigie kabla sijatuma kupitia namba hiyo ya kwanza. Simu ilipokelewa lakini sioni akiongea. Kwa vile sikuwa na shaka nikasema ngoja nimtumie, wakati namtumia likaja jina hili  “ FAJE  VJAGE”. Nikapata wasiwasi najina maana jina ninalolijua siyo hilo, nikamuuliza kwa sms.


Kabla sijapata jibu, likaja wazo kakangu ana namba ya voda ambayo kwa mjibu wake amesema haina chaji nikajaribu kupiga ikaita. Nikamsalimia tukaendelea na mazungumzo sikuona kama anazungumzia swala la pesa ikanilazimu nimuulize kama amenitumia sms yeyote. Akakataa, nikamusomea ujumbe ndipo akaniambia ni tapeli hata yeye ametumiwa ujumbe unaofanana na huo.

Yule tapeli akajibu swali langu la jina na kuniambia “ni lenyewe ametumia namba ya mtu mwenye jina hilo, pole bwana mdogo”. Hapa nilishajua huyu ni tapeli. Namba ya airtel imesajiliwa kwa jina la “FRANK JEREMIA”. Hiyo ilikuwa yapata saa sita mchana, usiku huu nimempigia kwa namba nyingine na kubali sauti akapokea lakini sijaweza kubaini sauti yake lakini kajitambulisha kwa jina la JOSEPH ANGELO yuko ARUSHA. Jina hili na eneo nahisi kanidanganya, hisia zangu ni kuwa tapeli huyu yupo Iringa maana ndipo kakangu alipo na mimi mwenyeji wa huko. Sina hakika kama mitandao inahusika labda mwenye utaalamu anaweza kutujuza.


Inasemekana ameshawatumia sms zinazofanana na hizi watu wengi tu, na inasemekana alianza mwishoni mwa mwaka jana na anaendelea. Sasa tapeli kama huyu tunawezaje kumkamata, kwa kupitia usajili wa simu au njia nyingine?

 

Nawasilisha kwenu nikitanguliza shukurani.


--




To all the questions of your life YOU are the  most possible answer. To all the problems of your life YOU are the best solution. Trust yourself

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CALj74g5rYUxuDpGHwaPen6Mp64tDcChn_uCwfsCFivzFPUQUZw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments