Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi mnono.
Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu mbili kubwa.
Kwanza, kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita, CCM wameingia katika uchaguzi huu wakiwa na mtaji mkubwa wa kusaidiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushinda, pamoja na jeshi la polisi.
Aidha, CCM wamengia katika uchaguzi huu huku serikali kwa ujumla wake ikiwa upande wake. Ushahidi wa hilo, ni nyaraka hii hapa ninayoibandika hapa.
Pili, washindani wakuu wa CCM – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeingia katika uchaguzi kikiwa kimekatika vipande viwili kutokana na mgogoro wa uongozi kati ya Zitto Kabwe na wenzake kwe nye chama.
Ni mwendawazimu tu, anayeweza kusema mgogoro ndani ya Chadema haukukiathiri chama hicho. Hamuwezi kuingia katika uchaguzi na mkategemea kushinda, wakati hamko wamoja; hamuwezi kuingia katika uchaguzi wakati wapenzi na washabiki wenu wakiwa wamegawanyika. Haiwezekani.
Kuingia katika uchaguzi katika mazingira hayo, matokeo yake ni hayo.
Kwa msingi huo, ili CCM kiweze kung'olewa kwenye madaraka
Kwa msingi huo, ili CCM kiweze kuondolewa madarakani, sharti Chadema kuwe na amani. Sharti NEC isiwe tawi la CCM kama ilivyo sasa.
Vinginevyo, miaka nenda rudi, CCM kitaendelea kutawala,wakati tayari kimekubwa na mchoko.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments