[wanabidii] KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014

Wednesday, February 05, 2014
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013. Ili kutekeleza azma hii tumeweka fomu kwenye tovuti ambayo wahitimu watarajiwa wa kidato cha sita wa mwaka 2014 watajaza kabla ya kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita. Baada ya kujazwa kikamilifu wakabidhi fomu kwa wakuu wa shule ambao 
watazirejeshe kwa Makamada wa Polisi wa mikoa kabla ya tarehe 17.03.2014. Wahitimu wa kidato cha nne wasijaze fomu hizi walishajaza kupitia "selform" walizojaza walipokuwa shuleni.

MASHARTI KWA MWOMBAJI:
  1. Mwombaji anatakiwa ajaze fomu hii kikamilifu na abandike picha yake "Passport Size" kwenye fomu kisha akabidhi kwa Mkuu wa Shule kwa hatua zaidi.

  2. Kila mwombaji aandike namba ya simu kwa usahihi na anuani yake ya kudumu ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.

  3. Bofya hapa kupakua Fomu ya Chaguo

Imetolewa na:
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments