"Kimya kimya msidhani; Ni ishara ya amani" - JK Nyerere - Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania ... mistari hii ya mashairi ndo dibaji ya kitabu hiki alichoandika Mwalimu kujadili suala la kudai Utanganyika. Na ingawa kipindi kile Mwl Nyerere alizungumzia serikali mbili lakini pia mistari hii imenifanya niwaze leo hii: kimya hii ni kuhusu nini. Kwangu ni kwamba kimya hii ni kuhusu vitu ambavyo hatutaki kutambua au kuviona na tunajidanganya eti tuna amani.. ni pamoja na utofauti mkubwa wa maisha, wananchi kukosa huduma za kijamii kama afya na elimu, ufujaji wa pesa.. Hatuandamani wala kupiga kelele sana lakini kimya hiki kina kishindo. Chonde chonde! Tusije tukawa mateka wa wanasiasa na kujikita katika muundo wa serikali na kusahau kilichotusukuma kudai na kuandika katiba mpya - kuboresha maisha yetu kama watanzania...
-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments