[wanabidii] Katibu wa CHADEMA Simanjiro atangaza mgogoro na kaimu mkuu wa wilaya ya Simanjiro

Monday, February 24, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO-CHADEMA WILAYA YA SIMANJIRO,
tunatangaza mgogoro na Kaimu mkuu wa Wilaya ya Simanjiro kwa hatua yake ya kutaka kuvifuta vitogoji Viwili kwa maana ya kitongoji cha #Tilili kilichoko kijiji cha Orbili kata ya Shamabarai na Kitongoji cha #Okutu kilichoko kijiji cha Okutu kata ya Naberera.

Tuna taarifa kuwa uwamuzi huu umefikiwa kwa shinikizo la CCM, kutokana na kutokuwa na mfuasi hata mmoja kwenye Vitongoji hivi viwili na sasa baadhi ya viongozi na makada wanazunguka kuwambia wananchi kuwa wasipokubali kujiunga na ccm watahamishwa kwenye maeneo ya CCM.

huu ni uhuni wa hali ya juu na ubakaji wa Demokrasia ambayo sisi kama CHADEMA hatuta kubali litokee kwa wanachama wetu na wana simanjiro kwa ujumla.

CHADEMA SIMANJIRO tunamuonya kaimu mkuu wa Wilaya asijaribu kuvunja katiba kwa Shinikizo la chama cha mapinduzi kwani ni haki ya kila raia wa Tanzania kuishi kwenye eneo lolote la jamuhuri ya muungano bila kujali kabila wala Dini yake.

Pia tunatoa Rai kwa wananchi wa Tilili na Okutu kuwa wasikubali kuhamishwa kwenye maeneo yao kwani hakuna sababu za Msingi za wao kuhamishwa.

Imetolewa leo Jumatatu, 24 Feb, 2014, Simanjiro na;

Frank Oleleshwa

Katibu (W) CHADEMA

0766265709

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments