[wanabidii] Je Polisi wa nchi hii wamespecialize kuwashtaki Chadema tu?

Friday, February 07, 2014
Kasi ya kuwashtaki viongozi na wanachama wa Chadema imepamba moto. Kasi hii huwa inatisha zaidi kipindi cha Uchaguzi. Kipindi hiki hata mfuasi wa Chadema akipigwa mpaka kutolewa meno atashtakiwa yeye badala ya yule aliyempiga na hasa kama kapigwa na Walinzi wa Kijani.

Je Polisi wamepewa maagizo maalumu ya kuhakikisha wanawashtaki Chadema kipindi hiki cha Uchaguzi ili kuwahujumu?

Kwanini Polisi wanaona kuwashtaki Chadema ni Priority kuliko kuwasaka waliorusha Hand Grenade kwenye mkutano wa Chadema wa Arusha na kuua watu wasio na hatia?

Je kwa Polisi kuwashtaki Chadema ni kipaumbele kuliko kumpata aliyempiga Dr Ulimboka baada ya juhudi za kumbambikia mgonjwa wa akili kushindikana?

Je kwa Polisi kuwashtaki Chadema ni priority kuliko kuwakamata madereva wa malori yanayosababisha ajali zinazoua Watanzania wasio na hatia kila wiki?

Halafu kwa ndugu zangu waandishi wa habari, je kesi ya Polisi aliyemwua Daudi Mwangosi inaendelea? 

Share this :

Related Posts

0 Comments