Ukimuona kwa Mara ya Kwanza kwa jinsi alivyo alivyo unaweza mchukulia poa sana kijana Amani Paul
Nilifahamiana na Amani Zaidi ya Miaka 8 iliyopita alipokuwa yuko chuo Kikuaa cha Dar-es-Salaam, wakati huo akiwa ametokea Shule ya Vijana wenye Vipaji Ilboru mkoani Arusha.
Mara baada ya Kumaliza Masomo yake ya Chuo Kikuu alinieleza kuwa hajisikii kuajiriwa anatafakari namna ya kuendesha maisha yake pasipo kuajiriwa. Aliniambia kama Watu wapo wengi wanaoishi pasipo kuajiriwa na hawajakwenda mpaka vyuo vikuu je si zaidi sana yeye??Mwaka 2007 tukaanza kufanya kazi na Amani katika Kampuni ya MANCON wakati huo tukiwa na Gazeti la "Gospel Today" yeye pamoja na swahiba Prosper Mwakitalima wakiwa ndio Wasimamizi Wakuu wa Gazeti hilo. Baada ya Miaka miwili baadae akaanzisha kampuni yake ya IT Farm akiwa kama mmoja wa Directors kazi yake kubwa ikiwa ni ku develop software kwa ajili ya mashule, Makanisa na Makumpuni Binafsi. Alipoanza kufanya kazi hiyo ikaanza kupata mafanikio mwaka 2011 akaanzisha Kampuni dada kwa ajili ya Video and Tv Productions ndipo kwa mara ya kwanza nikapata wazo la kuwa na kipindi cha TV nikiwa na Amani.
Mwaka 2011 nikiwa na Amani, James Temu na Christina Shusho tukapata wazo la Kukusanya Wakristo kukaa mahali kwa ajili ya Kupata Burudani ya Muziki wa Injili na Mambo mengine, tukakusanya marafiki wengine tukakaa kama Kamati kuona tunafanya nini, Issue ikaja hiyo Event Tuite jina gani??kila mtu akatoa wazo lake ndipo Amani akasema nashauri iitwe "Friends On Friday" mpaka leo hiyo event inaitwa "Friends On Friday" Jina alilotoa Mr. Amani Paul.
Baada ya Friends On Friday Kutimiza Mwaka Mmoja Amani Paul aliamua kuondoka Jijini Dar-es-Salaam na Kwenda Kuishi Kijijini kwao huko Hydom. Tulimshangaa sana sisi marafiki zake lakini akaamua kuwaza tofauti na kufanya Tofauti akiwa Hydom amani akaanzisha gazeti linaitwa OHAYODA lilikowa linaandika habari za huko kwao Mpaka sasa gazeti linaendelea vema na sasa linakuja na sura ya Mwana Jamii, akiwa huko huko Hydoma Amani Paul akapata Wazo la Kuandaa Tamasha la Utamaduni litakalokuwa likionesha Utamaduni wa Watu wa Huko Kwao ili uweze kutambulisha Tamasha hilo lilianza kwa hali ya changamoto kwa sababu ni kitu kipya Kijijini lakini baada ya mwaka mmoja mmoja Tamasha limekuwa na mafanikio makubwa kiasi cha Kutambulika na Wizara ya Maliasili na Utalii.unaweza pata detail kupitia www.ohayoda.blogspot.com
Mwaka 2014 Amani Paul Gesari Nanagi kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ameingizwa katika Kura za Vijana Wabunifuni Tanzania wenye ku promote Utalii wa Nchi ambapo mashindano hayo sasa yamefikia katika ngazi ya Taifa. Amani ni Kijana aliyeamua kupromote Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa Vision aliyonayo ni Kutaka Kuutangaza Utamaduni huu Nje ya Mipaka ya Tanzania. Wewe unayo Sehemu ya Ku-Support Amani afike anakotaka kwenda.
Chukua Simu Yako andika Sms neno C1 kisha tuma 15678 utakuwa umempigia simu Amani Paul piga mara nyingi uwezavyo utakatwa fedha ya kawaida.
Watu wenye Nguvu Huwainua wengine, Muinue Amani Paul.
--
Posted By Blogger to Sam Sasali Ze Blogger at 2/18/2014 09:25:00 AM
0 Comments