[wanabidii] CHADEMA MPANDA KIMESAMBALATIKA KABISA

Monday, February 24, 2014
Chadema mkoani Katavi kimewasimamisha uongozi viongozi wakuu wawili na wenzao wanne.

Waliosimamishwa uongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Katavi, Malack, Katibu Mwenezi wa chama hicho mkoani hapa ,

Sababu za kusimamishwa zimetajwa kuwa ni kuwakashifu viongozi wakuu wa Kitaifa, Mnyika na Lema katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mpanda mwezi uliopita.

Matongo na Mwenyekiti wa Jimbo la Mpanda Mjini, Seif Sipia. Wengine ni Katibu Mwenezi wa Jimbo la Mpanda Mjini Joseph Mona, ambaye pia ndiye Katibu wa Mbunge, Arfi na Katibu Mwenezi wa Jimbo la Mpanda Mjini, Godfrey Kapufi. Kapufi na Diwani wa Kata ya Makanyagio, Idd Nziguye mbali ya kusimamishwa uongozi, kikao hicho kimependekeza wavuliwe uachama kabisa kama ilivyokuwa kwa akina Dk Mkumbo na Mwigamba.

Aidha, kikao hicho pia kiliazimia Arfi achunguzwe wakimtuhumu kudhamini mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Maridadi mjini hapa unaodaiwa kutumika kuwakashifu Lema na Mnyika. Uamuzi huo mzito ulifikiwa katika kikao hicho kilichofanyika jana kwenye ofisi zilizopo katika mtaa wa Mji wa Zamani mjini hapa kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Magharibi, Masanja Katabi.

Ulinzi mkali wa walinzi wengi wa chama hicho uliowekwa wakati kikao hicho kikiendelea na Mwenyekiti wa jimbo la Mpanda Mjini, Sipia alilazimika kuhoji uhalali wa kikao hicho kwa madai wajumbe wake wengi hawakuwa wajumbe halali wa kikao hicho. Kutokana na hoja hiyo Mwenyekiti wa kikao hicho, Katabi alimuamuru Mwenyekiti huyo wa Jimbo atoke nje kwa kile alichodai kuwa analeta vurugu ndani ya kikao. Hata hivyo Sipia alikaidi agizo lake hilo ambapo vijana wa ulinzi wa chama hicho waliamriwa kuingia ndani ya kikako na kumwamuru Sipia atoke kwenye kikao hicho kwa nguvu. source HabairLeo 24/2/2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments