[wanabidii] VIGOGO CHADEMA WAANZA KUMCHAFUA WAKILI ALBERT MSANDO

Friday, January 17, 2014
Kile kikundi kinachosadikiwa kungwamkono na Viongozi wa Juu CHADEMA na kutumika kumchafua ZITTO sasa kimeanza kazi ya kumchafua mwanasheria MSOMI Alberto Msando

"Ukitaka kuwa na kichwa cha mwendawazimu kuwa mwanasiasa,

Ukitaka ufanyiwe njama, majungu na chuki za aina mbalimbali ongea ukweli.

By: Haule Zarafi zekitabu@gmail.com

Leo nimeshtushwa na kushangazwa na habari kwamba 'Wakili Msomi Albert Msando akamatwa na Magari ya wizi na nimeachiwa baada ya kutoa Mil 27'.

Habari hiyo imewekwa huko Jamii Forum na mtu anayejiita 'Recipient'.

Nimesema mara nyingi siasa sio mchezo mchafu sisi ndio wachafu.

Katika maisha hakuna kitu kibaya kama kukosa shukrani. Ni dhambi kubwa sana kuwa muongo na mnafiki. Ila Mungu huwa ana njia zake za kutaka ukweli ujulikane.

Taarifa za mpango wa kuanza kunichafua zilinifikia kupitia mtu ambaye katika maisha yangu ningeweza kumdharau na kumuona hana maana. Lakini kutokana na tabia yangu ya kutokumdharau mtu kwa sababu ya nafasi yake katika jamii mtu mmoja alinitafuta na kuniambia 'kaka Albert mimi sio mwanasiasa na sio mfuasi wa chama chochote ila kuwa makini sana kwa sababu kuna watu wameamua kukuchafua na kuhakikisha wanakuharibia kazi yako'. Hiyo ilikuwa jana tu! Leo taarifa hiyo ya uongo imetolewa.

Namuamini Mungu na naamini siku zote ukweli utasimama. Wema hulipwa kwa ubaya. Ni maisha.

Kwa marafiki zangu waliosoma au kusikia habari hiyo naomba msiipe umuhimu wowote. Sijakamatwa na Polisi wala SINA gari ya wizi. Magari yangu yote kwa nyakati tofauti nimewapa viongozi mbalimbali wa kisiasa hususan Chadema. Haijawahi kusemwa mahali popote ni gari za wizi. Mpaka leo!!!

Nimesikitishwa sana na chuki, hasira na jazba kwa sababu ya siasa. Kwa jinsi ambavyo nafanya kazi yangu kwa bidii, kwa kiasi ambacho naipenda na kuithamini familia yangu sina sababu wala uthubutu tena wa kufanya jambo ambalo litawaletea aibu na huzuni. Kwa vile ambavyo nimejitoa kuwa sababu ya mabadiliko kwa wananchi wa Mabogini siwezi kuwaaibisha kwa kuwa na tamaa ya kumiliki magari ya wizi.

Hatuwezi kufanikiwa kama nchi endapo siasa zetu ni za chuki, fitna, uongo, ulaghai na ujanjaujanja. Kutofautiana mawazo au mtizamo ni jambo la kawaida endapo tu wote mna NIA thabiti na ya dhati kuhusu kutatua matatizo ya wananchi.

Mimi siwezi kuwa na kinyongo na mtu. Kuna Mbunge mmoja alisema 'Hii kesi tutashindwa kwa sababu Albert anahonga majaji'. Mbunge huyo alisahau kwamba nimewahi kutetea kesi tatu zinazowahusu watu wa karibu na kushinda bila kulipwa hata senti moja. Wakati huo hakusema nimehonga. Leo hii kwa busara zake akatamka maneno hayo. Nilimtumia ujumbe kwenye simu na kumwambia 'namuachia Mungu'.

Tusichukiane. Tuonyeshe ukomavu wa kisiasa. Chuki na fitna ni anguko letu sote.

Nimeonelea vyema niseme niliyoyasema. Nataka wale wanaotafakari kunichafua na kufanya ubaya wowote wajue kwamba wanachodhamiria kinajulikana na kinatarajiwa. ila yote nayaacha mikononi mwake Mungu wangu aliye hai. Atanilinda na kuniongoza.

AGM 2014.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments