[wanabidii] UTAFITI KUKUSANYA MAONI YA WAFANYABIASHARA KUHUSU ATHARI ZA UREJESHWAJI WA ADA YA LESENI ZA BIASHARA.

Friday, January 17, 2014
Na.Aron Msigwa – MAELEZO
Chama cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua rasmi utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS Mobile System) kuhusu madhara yatokanayo na urejeshwaji wa ada za biashara kila mwaka kwa lengo la kuishawishi serikali kuweka sera, sheria na taratibu rafiki kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini.

Akizungumzia utafiti huo leo jijini Dar es salaam Rais wa cha hicho Injinia Peter Chisawillo amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 serikali ilitangaza urejeshwaji wa ada ya leseni za biashara nchi nzima na kuongeza kuwa utaratibu huo unaomlazimu mfanyabiashara kukata leseni na kuilipia kila mwaka unakwenda kinyume na sheria ya leseni ya mwaka 1972.

Amesema kuwa sheria hiyo na hasa marekebisho yake ya mwaka 2004  yaliwezesha leseni za biashara kutolewa bure na mara moja tu kwa kipindi cha maisha yote ya biashara jambo ambalo linakiukwa.

"Tayari kuna malalamiko mengi kwa jumuiya ya wafanyabiashara yanayotufikia kutoka kuanzia ngazi za wilaya na mikoa juu ya urejeshwaji wa ada hiyo, sekta binafsi inailalamikia serikali kwa kutoishirikisha katika urejeshaji wa utaratibu huu ambao unaiathiri sekta hii moja kwa moja" amesema Injinia Chisawillo.

Ameeleza kuwa sekta binafsi inaamini kuwa serikali imeamua kuongeza mapato bila kuzingatia nia ya urasimishaji wa sekta isiyo rasmi kwa lengo la kuharakisha uchumi kwa ujumla na kuongeza kuwa hakuna mwongozo maalum uliotolewa na serikali kuelekeza namna maombi ya leseni yatakavyoshughulikiwa.

Amesema sekta binafsi inaamini kuwa ili kuondoa urasimu na usumbufu kwa wafanyabiashara pindi wanapoomba leseni kila mwaka , serikali itumie kumbukumbu zilezile kila mwaka bila kulazimu mfanyabiashara  kufuata mlolongo wa taratibu za kuomba leseni kila mwaka kwa lengo la kuokoa muda na kupunguza kupanda kwa gharama za uendeshaji wa biashara.

Aidha Injinia Chisawillo amesema kuwa utafiti huo unaofanywa na TCCIA) utafanyika kwa muda wa wiki 4 ukiwahusisha wanachama wote  takribani 22,000 (Elfu Ishirini na mbili) na wale wasio wanachama na unafadhiriwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la BEST –AC ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu zao kwenda namba 15539  na kutoa maoni kuhusu urejeshwaji wa ada hiyo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
2 Comments
avatar

Je, wewe ni matatizo ya kifedha au unahitaji fedha haraka ya kulipa bili yako? Na unataka kuchukua hatari ya kubadilisha maisha yako mwenyewe. Jaribu na kupata ATM tupu kadi yako leo na kuwa miongoni mwa bahati ya mtu ambaye ni kunufaika na kadi hii. Kadi hii ATM ni kuweka uwezo wa Hacking katika mashine yoyote ATM popote duniani. Nina kujua kuhusu kadi hii tupu ATM wakati mimi nilikuwa kutafuta kazi online kama mwezi mmoja uliopita. Ni kweli iliyopita maisha yangu milele na sasa siwezi kusema mimi nina tajiri kwa sababu mimi ni ushahidi hai. fedha kidogo mimi kupata katika siku na kadi hii ni $ 3,000. Hata sasa na kisha kuweka kusukumia fedha katika akaunti yangu. Ingawa kadi ni kinyume cha sheria lakini hakuna hatari ya kuwa hawakupata. Ni iliyowekwa katika namna ambayo haiwezi kupatikana na pia ina mbinu ambayo inafanya kuwa vigumu kwa CCTV kamera ya kuchunguza wewe wakati wa kutumia hiyo. Kwa maelezo juu ya jinsi ya kupata yako leo mawasiliano speedhackersnetwork001@gmail.com

REPLY
avatar

Are you suffering financially or do you need an urgent cash to pay your bills? And you want to take the risk of transforming your own life. Try and get your ATM blank card today and be among the lucky one's who are benefiting from this card. This ATM card is set capable of hacking into any ATM machines anywhere in the world. I have to know about this blank ATM card when I was looking for work online about a month ago. It has really changed my life forever and now I can say I'm rich because I am a living testimony. The less money I get in a day with this card is $3,000. Even now and then keep pumping money into my account. Although the card is illegal but there is no risk of being caught. It is programmed in such a way that it cannot be tracked and also has a technique that makes it impossible for the CCTV camera to detect you when using it. For details on how to get yours today contact speedhackersnetwork001@gmail.com

REPLY