[wanabidii] TRA mnatunyonya kwa hii ya malipo

Monday, January 13, 2014
Ndugu wadau wa hili jamvi kuna mambo ambayo sijui ni serikali au TRA wameyaingiza kwenye mfumo wa ulipaji huduma au manunuzi ambapo mtu ukinunua bidhaa na ukaamua kumwandikia suppliyer wako cheki au Tiss inakatwa kitu wanaita excesice duty ya 0.15% ya malipo uliyofanya. Tiss ndio inakatwa mara mbili hiyo 0.15 %ya TRA na sh. 10,000 BOT.
 Hii sioni kama ni halali ni unyonyaji wa fedha zetu kwani tunaponunua tunalipa VAT, na ukiuza ulichonunu faida yake unalipia tena kodi ya asilimia 30. Sasa iweje ninapomlipa kwa cheki aliyeniuzia huu mzigo ambao umeshakatwa kodi zote hizo hiyo cheki nayo ikatwe tena asilimia 0.15 ?  jamani mnakotupeleka siko. Sasa hivi hata ukilipia  maji,  umeme au ada ya shule, n.k kwa cheki au mitandao ya simu asilimia hiyo inakatwa licha ya kodi nyingine zinazokuwa zimekatwa tayari .
Jamani huu ni wizi sasa TRA wanatufanya sasa tufanye malipo ya cash mikononi ili kukwepa hizo garama zao. Jamani watetezi wa hili jambo ni mimi na wewe inabidii tulipaazie sauti zetu, mwishowe tutalipishwa kodi ya asilimia fulani kwa hewa tunayovuta.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments