[wanabidii] HATARI HII ISIACHWE IKALETA MAZOEA MABAYA KWA TAIFA

Sunday, January 12, 2014
Ndugu,
Awali ya yote naomba nichukuwe nafasi hii kutoa pongezi zangu kwa serikali na chama tawala kwa kuwa tayari kuendana na upepo wa msukumo wa kisiasa nchini hatimaye kuwajibishana na kufikia hatua ya kuwaondoa viongozi ambao wizara zao zimefanya vibaya ama kwa kutokutimiza malengo tarajiwa katika jamii au kutokana na madhambi yaliyofanyika katika jamii ya watanzania ambayo yametokana na utekelezaji wa maagizo yanayotoka katika wizara zao.
Tukumbuke kuwa jamii imetutuma kuwatumikia na hatimaye kuwasaidia kujiletea maendeleo,hivyo ni jukumu la serikali kuwahakikishia usalama wao na kufanya yale ambayo wao wataona yanawafaa na si vinginevyo.
Serikali na Taifa kwa ujumla linakabiliwa na changamoto ya kubadilisha badilisha viongozi wa juu kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea katika nchi yetu, sio dhambi kubadili viongozi ni utaratibu mzuri lakini changamoto inakuja ni kwa namna gani au msukumo gani unatupelekea kufanya mabadiliko haya, na kwa faida ya umma au ya watu wachache ambao wamechagiza kuleta mabadiliko hayo. Haya yote yanatutaka kufikiri kwa makini ili siku zote mabadiliko yasilenge kumuonea mtu, kumvunjia heshima au pia kumpendelea mtu ama kundi fulani. Tusipokuwa makini basi hata anayefanya mabadiliko hayo mathalan mh rais anaweza kujikuta akishiriki kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa baadhi ya viongozi wanaoingia madarakani au waliobahatika kubaki katika nafasi zao kwa hofu ya kuondolewa katika nyazifa zao ama kwa kutowapendeza wachache au kufanya maamuzi magumu ambayo wakati fulani yanaweza kuleta manufaa kwa umma lakini hasara kwa wachache.
Ukitafakari mfumo wa utawala wa nchi yetu utagundua kuwa hata kama utakuwa na kiongozi mwenye weredi kiasi gani, awe ametoka chama gani lakini mfumo uliopo unaweza kumuwajibisha na akaonekana hajafaa kuvaa viatu vya wizara hiyo. Ninadiriki kusema hivi kwa sababu wapo mawaziri wengi wananyooshewa vidole kuwa ni mizigo, na wengine wamediliki kumnyooshea kidole mpaka waziri mkuu, sina uhakika kama ni kweli hawa hawana sifa au wameshindwa wote ingawa inawezekana kabisa wakawa na kasoro ndogondogo katika uongozi wao. Serikali na chama tawala kwa ujumla visipokuwa makini siku moja baadhi ya wananchi na hata wanachama wa chama tawala wanaweza kumnyooshea kidole mh Rais na kusema hafai na awajibike, je hatuoni kama itakuwa ni hatari au matusi kwake yeye na kwa wananchi waliomchagua?
Lakini tujiulize kwa makini je ni kweli kila anapowajibishwa waziri fulani anakuwa amehusika moja kwa moja na sababu zinazompelekea kuwajibika?
Viongozi walio chini yake ambao ndio watendaji wakuu wanakuwa wasafi kiasi gani wakati waziri anawajibishwa?
Je ni kweli lazima waziri awajibike kirahisi tu hata kama makosa sio yake moja kwa moja yeye kama waziri?
Nimetafakari kwa makini ndio maana nikaona utaratibu huu siku moja unaweza kutufikisha katika maamuzi ambayo yanaweza kuwaondoa viongozi ambao wanatufaa lakini kutokana na uzembe wa baadhi ya watendaji waliopewa jukumu la kushiriki kufanya maamuzi ya serikali na chama kwa vitendo kutokuwa na uwezo au kufanya vibaya kwa makusudi,hii inawezekana sana hasa kipindi hiki kwa kuwa baadhi ya watendaji wanaendekeza itikadi wanazozijua wao ama kwa kuwa wao ni wafuasi wa vyama vya upinzani au basi tu wao ni destuli yao kila mpango utajimalizikia wenyewe bila ya wahusika kufikiri kutumia taaluma zao vema ili kuleta tija katika utekelezaji wa shughuli zao.
Kwa kuzingatia haya yote ndio maana serikali na chama kwa ujumla lazima ifikie hatua ya kutafuta suluhisho la tatizo hili kwa vitendo ili pamoja na mabadiliko ambayo lazima yafanyike utafutwe mfumo madhubuti wa kusimamia maamuzi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za watendaji ili kuongeza tija na katika utekelezaji wa mambo mbalimbali kwa manufaa ya umma. Mfumo ambao hautasubiri ziara za viongozi wa serikali, upinzani au chama tawala ili kuzungumzia kero ya baadhi ya watendaji wa serikali kwa wananchi,mfumo ambao utawafanya watendaji kuwa na msukumo wa kuwatumikia wananchi kwa vitendo na sio kukaa maofisini tu.
Ninapendekeza kiundwe chombo huru mpaka katika ngazi ya mikoa na baadhi ya wajumbe wake wawe wenye muelekeo wa kupenda na kulinda utekelezaji wa ilani ya chama tawala ili yale yote yaliyomo kwenye ilani basi yatekelezwe kwa vitendo kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo. Ni wazi kuwa bila kufanya hivi siku moja tutaangaliana kwa mshangao kwani serikali yaweza kuonekana kama bendera ambayo inafuata upepo.
Huu ni wakati muafaka kwa mh rais kuangalia namna ya kufanya ili kuzima moto huu ambao unashika kasi. Ianzishwe namna ambayo itapima maamuzi mbalimbali na utekelezaji wa mipango ya chama na serikali kwa taifa la Tanzania ili ijapotokea changamoto katika utekelezaje basi kuwe na chombo kitakachobainisha mhusika/wahusika ili ichukuliwe hatua stahiki. Siasa ni sanaa itumike vema "the aim of art is to represent not the outward appearance of things, but their inward significance –aristotle".

Mwl John kamunu mniko,
0758044254/0714229939
kamunukamunu@yahoo.com
kidumu chama cha mapinduzi 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments