[wanabidii] FURSA/OPPORTUNITIES

Thursday, January 09, 2014
Ndugu Zangu Watanzania, Heri ya mwaka 2014!

Hivi karibuni kumekuwa na muamko wa kuhamasishana katika kutafuta na kubuni Fursa miongoni mwa sisi Watanzania. Jambo zuri na la kuliendeleza kwani litaleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wengi na kwa Taifa kwa ujumla.

Umeshawaza kuwekeza kwenye Ardhi katika mfumo wa kiwanja au shamba – Maeneo ya Bagamoyo mpaka Msata?
Kama ni ndiyo basi habari ifuatayo itakufaa.
Kuna viwanja (Surveyed Plots) zinauzwa Tshs. 13,500.00 kwa meta moja ya mraba ( TZS 13500.00 per square meter). Viwanja hivi vipo 6 km kabla ya kuingia Bagamoyo mjini ukitokea Dar es Salaam, upande wa kushoto. Eneo hilo linaitwa Mataya. Ramani ndogo pamoja na chati inayoonyesha viwanja hivyo pamoja na ukubwa wake imeambatanishwa.
Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba +255 754 787 775 au +255 655 787 775. Email address – gck@ksonsfreight.co.tz au info@ksonsfreight.co.tz.

Kwa nini ufikirie kununua kiwanja au eneo pande za Bagamoyo zaidi ya maeneo mengine?
Bandari ya Bagamoyo (SEAPORT) na Export Processing Zone (EPZ)
Bandari kubwa ya mizigo itaanza kujengwa hivi karibuni kule Bagamoyo. Kumekuwa na ongezeko la ya Import na Export ndani ya Nchi na Nchi jirani. Bandari hiyo itakuwa busy sana.
Karibu na bandari hiyo kumetengwa eneo kwa ajili ya viwanda vitakavyozalisha au kuboresha bidhaa kwa ajili ya soko la nje ya Nchi [Export Processing Zone (EPZ)]. Pilika pilika za kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi zimeshaanza.

Nini cha kutegemewa?
Somo la Jiografia linasema Bandari na Viwanda ni kati ya vitu vinavyochangia sana ukuaji wa miji (makazi ya watu) pamoja na shughuli za kimaendeleo!
Bandari pamoja na EPZ zitahitaji wafanyakazi wengi sana na wa aina zote kuanzia wakati wa kujenga mpaka kuendesha miradi yenyewe.
Mahitaji yatanzania kwenye Makazi, Maduka, Shule/Vyuo, Nyumba za kupanga/kulala wageni, Karakana/garage za aina zote n.k. Iwe ni bustani ya matunda au mboga, shamba la mihogo au viazi, nyumba za kupangisha au kulala wageni, maduka (supermarket), vyote hivyo vitakuwa biashara.
Una kiwanja au eneo lakini umekosa kabisa namna ya kuwekeza, natumaini utapata muwekezaji wa kuingia naye ubia au kupanga kwenye kiwanja au eneo lako. Na kadhalika, na kadhalika.

Uzoefu kidogo nilioupata.
Mwaka 2009, eneo fulani karibu na Msata liliuzwa ekari moja kwa Tshs 200,000.00. Miaka Miwili baadaye (2011) bei ya ekari moja ilipanda kutoka Tshs 200,000.00 na kufikia Tshs 1,000,000.00.
Ongezeko la 400% bila stress wala kuhangaika!! Sijui kwa leo hii 2014 bei inaweza kuwa imefika kiasi gani!

Wageni wameanza kunyemelea na kunyakua maeneo hayo kwa kasi.
Mchina mmoja ameniambia kwamba Wachina wengi wananunua viwanja au maeneo pande za Bagamoyo wakivizia fursa zinazotarajiwa.
Sina kinyongo na Wachina kuwekeza (kwenye kazi halali na stahiki) hapa nchini, lakini je, sisi tuendelee kubaki kuwa watazamaji tu? Au nasi tujitose kama ambavyo wengine wametangulia??

Nawatakieni heri na mafanikio mwaka 2014 na kuendelea!

Kigolla.





Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments